Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha rasilimali za Ziwa Victoria zinalindwa ili zinufaishe jamii zinazozunguka ziwa hilo na mataifa husika.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe kutoka Tanzania katika mkutano
huo wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa
Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika
ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 19 Aprili, 2023 jijini Kampala,
Uganda.
Prof. Shemdoe alisisitiza kuwa Tanzania inaendelea
kudhibiti matumizi ya zana haramu za uvuvi, kupiga marufuku uvuvi wa samaki wachanga,
kudhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi na kuhamasisha ufugaji wa samaki kwa vizimba
katika Ziwa Victoria bila kuathiri mazingira.
Pia alisema kuwa Tanzania imeimarisha udhibiti wa uingizwaji
wa zana haramu za uvuvi na kuendesha ukaguzi wa kina ili kuhakikisha kunakuwa
na uvuvi endelevu na wenye tija.
Mchango wa Sekta ya Uvuvi katika uchumi wan chi za Jumuiya
ya Africa Mashariki bado ni mdogo kwa kuwa mchango wake haujumuishwi na mapato
yanayotokana na shughuli zote za uvuvi zinazofanyika katika mnyororo wa thamani
badala yake mchango huo unaotokana na mnyororo wa thamani unajumuishwa katika
sekta nyingine.
Mkutano huo umehudhuriwa nan chi wanachama wa Jumuiya ya
Africa Mashariki (EAC) zilizopo katika Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni