Na Mbaraka Kambona, Singida Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesema kuwa Serikali imedhamiria kulitumia eneo la kupumzishia mifugo la Kitaraka lililopo wilayani Manyoni, Singida liweze kutumiwa na vijana watakao hitimu mafunzo katika vituo atamizi kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo kibiashara ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla. Mhe. Ulega alibainisha hayo wakati wa kikao baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Peter Serukamba (kushoto) alipokutana nae katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida Januari 30, 2023. Wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Ulega alimueleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa lengo la ziara yake ni kujadiliana nae kuhusu dhamira ya Serikali ya kutaka kulitumia eneo la kitaraka kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mifugo ili kuwawezesha vijana kujipatia ajira lakini pia kuzalisha malighafi ya uhakika kwa ajili ya viwanda vya nyama na kuifanya sekta ya mifugo kuchangia ipasa...