Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Uvuvi) imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa usimamizi wa pamoja wa
rasilimali za uvuvi na mazingira ya bahari SWIOFIC -Nairobi Convention unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia
Shirika la Maendeleo la Kimataifa (SIDA)
Akizungumza mara baada ya
kupokea ripoti hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya
Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi
Tanzania (TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei, amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa
miaka mitano tangu 2019 na unatarajiwa kumalizika mwezi Disemba 2023
Amesema lengo la mradi
kuwezesha ushirikiano katika masuala ya usimamizi wa mazingira, kuimarisha
rasilimali za Uvuvi na kuboresha maisha ya jamii za wavuvi kwa ujumla
"Mradi huu unafanyika
kwa majaribio kwa upande wa Tanzania, Madagascar na Msumbiji, baada ya hapo
matokeo yatakayotokana na mradi huu yatatumika kama mfano katika nchi nyingine
hasa katika nchi za Magharibi mwa Bahari ya Hindi ambako utatekelezwa mradi
mkubwa zaidi" amesema
Ameeleza kuwa Serikali ya
awamu ya sita inaendelea na jitihada za kuboresha mazingira ya uvuvi hasa
Ukanda wa Pwani ikiwemo kuanzisha miradi mikubwa ya kuendeleza miradi ambayo
imekwisha muda wake
"Nia ni kuona
uzalishaji katika dhana pana ya uchumi wa bluu inafanya kazi na wananchi wetu
wanapata maboresho kwa maana ya kupata kipato na lishe bora kwa kuzingatia
usalama wa chakula ili kuinua uchumi wao binafsi na uchumu wa taifa kwa ujumla
Aidha amebainisha kuwa
pamoja na mambo mengine Serikali imeendelea na jitihada za kuboresha sekta ya
uvuvi ikiwemo kuanzisha ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko na Zanzibar
Amewataka wananchi na
wavuvi kuwa tayari kupokea fursa zote zinazoletwa kupitia miradi mbalimbali ili
kuungana na Serikali ya awamu ya sita ambayo imejikita pia katika kuendeleza
kutekeleza miradi hiyo pindi inapomalizika.
Mkurugenzi Mkuu kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei akiongea
wakati wa kufungua kikao cha kupokea
taarifa za utekelezaji wa mradi wa
SWIOFIC- Nairobi Convention
kilichofanyika Mkoani Tanga Januari 26,2023 lengo likiwa ni pamoja na
kuwezesha ushirikiano katika masuala ya usimamizi wa mazingira na Uvuvi Ili
kuimarisha usalama wa Chakula kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi
na kuimarisha maisha ya jamii za wavuvi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na washiriki wa kamati ya wataalam wa mradi wa SWIOFIC -Nairobi
Convention mara baada ya kikao cha kupokea taarifa za utekelezaji wa mradi huo
kilichofanyika Mkoani Tanga Januari 26, 2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni