Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2022

KAMBAMITI KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA KUKUZA SEKTA YA UVUVI - DKT. TAMATAMAH

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah amesema Rasilimali ya samaki aina ya kambamiti  ni muhimu katika kutoa ajira, kipato, chakula na lishe, na  kuliingizia Taifa fedha za kigeni kama aina nyingine za samaki na hivyo kuchangia katika kupunguza umaskini kwa wananchi. Dkt. Tamatamah aliyasema hayo wakati wa kikao na wakuu wa idara, Taasisi na Vitengo  wa sekta hiyo kujadili juu ya rasimu ya mpango wa usimamizi wa zao la kambamiti kilichofanyika jijini Dodoma Mei 23, 2022. Alisema wote tunafahamu kuwa, kabla ya mwaka 2007, uvuvi wa kambamiti ulikuwa ukifanywa na wavuvi wote wakubwa na wadogo, na mwaka 2007 uvuvi huo ulifungwa kwa wavuvi wakubwa kufuatia taarifa za utafiti zilizothibitisha kuendelea kupungua kwa rasilimali hiyo na hivyo kutisha uendelevu wake. Hivyo kufuatia changamoto hiyo mwaka 2012, Serikali iliandaa mpango wa usimamizi wa rasilimali ya kambamiti wa miaka mitano ulioanza kutekelezwa mwaka 2013 na kuisha muda wake  mwaka...

NDAKI AZINDUA ZOEZI LA UUZAJI MADUME BORA YA NG'OMBE NCHINI

Picha
Na Mbaraka Kambona,  Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imezindua zoezi la uuzaji wa madume bora ya ng'ombe aina ya Borani ili kuwawezesha Wafugaji nchini kuboresha mifugo yao ili iwe na tija zaidi kuliko hivi sasa ambapo wengi wana makundi makubwa ya ng'ombe huku tija yake ikiwa ni ndogo. Hafla fupi ya uzinduzi wa zoezi hilo la uuzaji wa madume bora ya ng'ombe aina ya Borani ilifanyika katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, jijini Dodoma Mei 21, 2022. Wakati akizindua zoezi hilo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi alisema anaimani kuwa uuzaji wa madume hayo bora kutasaidia wafugaji wengi kupata mbegu bora itakayosaidia kuboresha ufugaji wao. Alisema kuwa wafugaji ni vyema kutumia fursa hiyo vizuri na kuchangamkia madume hayo huku akiwataka kuamini kuwa na mifugo michache iliyobora ndio utajiri kuliko kuwa na kundi kubwa la ng'ombe ambalo tija yake ni ndogo. Aliendelea kuwakumbusha wafugaji kuwa wakiendelea kuamini kuwa na makundi maku...

MIRADI YA MAENDELEO MKURANGA IPO KATIKA HATUA NZURI - NZUNDA

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na uvuvi (Mifugo) Bw.Tixon Nzunda jana tarehe 20 Mei 2022 alifanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) Mkoani Pwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na kuridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa miradi hiyo mbali ya mapungufu madogomadogo aliyoelekeza kurekebishwa mara moja kabla ya kukamilisha miradi hiyo 30 Mei 2022 . "Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoendelea kufanya pamoja na kwamba ulipatwa na changamoto ya ajali lakini unaendela vizuri na utekelezaji wa mradi huu." Alisema Nzunda alipokuwa anakagua ujenzi wa kisima katika kijiji cha Matanzi. Miradi inayotekelezwa Katika Halmashauri ya Mkuranga inayosimamiwa Moja kwa moja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) ni pamoja na ujenzi wa Mnada wa Kisasa wa upili unaojengwa katika kijiji cha Chamgoi wenye thamani ya Tsh.  300, 274, 584.09 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 45.75. Aidha, mradi mwingine alioutembelea Katibu Mkuu Sek...

SERIKALI YAFICHUA ILIVYOPATA MWAROBAINI WA MAGONJWA YA MIFUGO NA MASOKO.

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka wazi namna ilivyofanikiwa kupata suluhu ya changamoto ya ukosefu wa masoko ya mazao ya Mifugo na uhaba wa chanjo za magonjwa mbalimbali ya Mifugo. Hayo yamebainishwa leo (20.05.2022)  na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia afya ya jamii ya veterinari, udhibiti wa pembejeo, mifugo na mazao yake kutoka Wizarani hapo ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu (Mifugo)  Dkt. Stanford Ndibalema wakati wa hotuba yake ya kufunga mafunzo ya Siku 3 ya mfumo wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirisha mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi unaojulikana kama “ Mifugo Management Information System (MIMIS)”  kwa wataalam na wadau waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya Mifugo na Uvuvi yaliyokuwa yaliyofanyika kwenye hoteli ya Royal Village jijini Dodoma. Dkt. Ndibalema amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika nchi za falme za kiarabu, Wizar...

WIZARA YAAHIDI KUANZA KUFANYA MAFUNZO KWA WAELIMISHA RIKA.

Picha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya uvuvi imeahidi kuanza kufanya mafunzo mbalimbali kwa waelimisha rika ambao watakuwa kiungo muhimu katika kutekeleza jitihada za kutokomeza Ukimwi, MSY na homa ya Ini mahala pa kazi. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah alipokuwa akizindua kamati ya VVU, Ukimwi na magonjwa sugu yasiyoambukizwa(MSY) mahali pa kazi, tukio hilo limefanyika leo (20.05.2022) kwenye ukumbi wa ofisi za wizara NBC, Dodoma.  " Sote tunafahamu kuwa Afya ya watumishi ndio msingi mkuu wa uendeshaji wa Taasisi yeyote. Hivyo, suala la afua za UKIMWI na MSY Mahali pa kazi lisipopewa kipaumbele, Utumishi wa umma unaweza kujikuta unapoteza nguvu kazi kutokana na magonjwa na vifo", amesema Dkt. Tamatamah. Dkt. Tamatamah ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora (OR-MUUUB), Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wameshirikiana na wizara...

ULEGA AHIMIZA ZAO LA DAGAA KWENDA KIMATAIFA

Picha
Na Mbaraka Kambona, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Kusafirisha Mizigo (DHL) nchini Tanzania, Bi. Fatma Abubakar kujadiliana namna Serikali na shirika hilo watakavyoweza kushirikiana  kufungua zaidi masoko ya Kimataifa ya  zao la Dagaa na Mwani. Waziri Ulega alikutana na Mkurugenzi Mtendaji huyo wa DHL  jijini Dodoma Mei 19, 2022. Akizungumza katika majadiliano yao hayo, Waziri Ulega alisema zao la dagaa kwa muda mrefu limekuwa likiuzwa katika nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika lakini biashara hiyo imekuwa ikifanywa kienyeji sana jambo ambalo limesababisha nchi na watu wake kutokuona tija kubwa ya zao hilo. "Pamoja na dagaa kuuzwa katika masoko ya nje bado watu wanafanya kienyeji sana, tunatakiwa tuwekeze katika kuliongezea thamani zao la dagaa na kulifungasha vizuri ili liweze kuthaminika katika masoko ya kimataifa na litanunuliwa kwa wingi kuliko ilivyo hivi sasa", alisema Aliongez...

KATIBU MKUU NZUNDA AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA VITUO VYA WAKALA YA MAABARA YA VETERINARI TANZANIA

Picha
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Tixon Nzunda leo Mei 19,2022 amekabidhi magari mawili kwa vituo vya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye mikoa ya Arusha na Tabora. Magari hayo yamenunuliwa na Wakala ya Maabara yya Veteinari Tanzania (TVLA) kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kama ilivyopangwa katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2021/20022. Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo katika Ofisi za TVLA Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Nzunda amevitaka vituo ambavyo vimekabidhiwa magari hayo waende wakayatumie magari hayo kwa shughuli za TVLA kwaajili ya mafunzo kwa wafugaji na wadau wao wanaozalisha chakula cha mifugo ili waweze kuongeza tija na kuongeza mapato zaidi kwa taasisi. "Tumieni magari haya kwaajili ya kutangaza shughuli za taasisi na shughuli za mifugo na kuwafikia wafugaji kwa ukaribu zaidi ili tuweze kutoa chanjo kwa wakati, chanjo zikiwa salama na kuwafikia wadau wengi zaidi lakini kuongeza wigo wa uto...

WAFUGAJI ACHENI KUTOROSHA MIFUGO KWENDA NCHI JIRANI-NZUNDA

Picha
Katibu Mkuu Mifugo Bw.Tixon Nzunda amekemea Vikali tabia ya wafugaji kutorosha Mifugo na kwenda kuuza nchi jirani ya Kenya kwa kukwepa kulipa Ushuru na  tozo halali za serikali. "Wafugaji wetu wanatorosha Mifugo na kwenda kuuza nchi jirani, kwa kukwepa kulipa tozo na Ushuru halali wa Serikali,wanapitisha Mifugo hiyo katika njia zisizo rasmi,na kibaya zaidi kuna baadhi ya watumishi wa Umma na Polisi wasiokuwa waaminifu wanashiriki utoroshaji huo. Alisema Nzunda" Hayo ameyasema jana 17 May 2022 alipokuwa Mkoani Tanga akikagua miradi mbalimbali ya  Maendeleo ya Sekta Mifugo. Nzunda amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Africa kuwa na Mifugo mingi ikitanguliwa na Ethiopia, lakini Sekta hiyo ya Mifugo inachangia asilimia 7.1 tu katika pato la Taifa,amewaasa wafugaji hao na watumishi wa Serikali wasiokuwa waaminifu wanaoshiriki zoezi la utorosha Mifugo nje ya nchi kuacha mara moja. "Unajua Sekta hii ya Mifugo inaweza kuchangia katika pato la taifa hata kwa asilimia 15 m...

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kuanza kutumia mfumo wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirisha mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi unaojulikana kama “ Mifugo Management Information System (MIMIS)” ambao unalenga kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara za Mifugo, kukata na kuhuisha leseni za wataalam wa Mifugo na vibali vinavyohusu uingizaji, uzalishaji na uuzaji  wa vyakula vya samaki. Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia sekta ya Mifugo Dkt. Charles Mhina alipokuwa akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo huo kwa wadau na wataalam kutoka sekta za  Mifugo na Uvuvi yaliyofanyika leo (18.05.2022) kwenye hoteli ya Royal Village jijini Dodoma. “Uwepo wa mfumo huu utatusaidia kuokoa muda wa kushughulikia vibali lakini pia utaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuokoa fedha za Serikali  kwa sababu “Control Number” itazalishwa pale mtu anapofanya maombi tofauti na sasa ambapo mtu a...

BILIONI 5 KUTUMIKA KULINDA HIFADHI ZA BAHARI NCHINI

Picha
Na Mbaraka Kambona,  Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) wamekubaliana kutekeleza Mradi wa kulinda na  kutunza baianuai ya ukanda wa Bahari ya Hindi katika Wilaya ya Mkinga iliyopo Mkoani Tanga. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki alibainisha hayo baada ya kufanya kikao kifupi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Dkt. Katrina Bornemann kilichofanyika ofisini kwake  jijini Dodoma Mei 18, 2022. Alisema lengo la mradi huo ambao utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 5 ni kuhakikisha maeneo ya bahari pamoja na ukanda wa pwani Wilayani Mkinga yanalindwa na kuhifadhiwa ili yaweze kuwa endelevu na kuleta maendeleo kwa wananchi. "GIZ wamekubali kutoka kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 5 kwa ajili ya kutunza mazalia ya samaki, maeneo tengefu na fukwe za bahari ili maeneo hayo yaweze kuwa na tija zaidi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla", alisema Aliongeza kwa kusema kuwa  wameshakubaliana mradi huo ...

SERIKALI YAWATANGAZIA VITA WAVUVI HARAMU

Picha
Na Mbaraka Kambona, Mwanza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema serikali sasa itawekeza nguvu kubwa kukomesha uvuvi haramu katika ziwa viktoria baada ya hatua kadhaa zilizochukuliwa hapo awali ikiwemo kuwashirikisha wavuvi wa kanda ya ziwa kutokuzaa matunda. Ndaki alitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya uvuvi katika kikao cha kujadili changamoto wanazokabiliana nazo wavuvi wanaofanya shughuli zao katika ziwa Viktoria kilichofanyika Mkoani Mwanza Mei 16, 2022. Alisema mwaka jana serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya uvuvi waliandaa mpango shirikishi ambao ulianisha kila mdau na jukumu lake katika ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa viktoria lakini matokeo yake wadau hao hawakujali na sasa uvuvi haramu umeongezeka maradufu. “Uvuvi haramu sasa hivi ni mkubwa kwenye ukanda wetu wa ziwa viktoria, na sisi wizara tumepewa jukumu la kusimamia rasilimali hizi, Mhe. Rais atatushangaa sana kuona wizara iliyopewa dhamana ya kuhakikisha rasilimali ...

SEKTA YA UVUVI KUANDAA DAFTARI LA VIASHIRIA HATARISHI

Picha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Sekta ya Uvuvi imeanza kuandaa daftari la viashiria hatarishi katika sekta ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 iliyofanyiwa marekebosho mwaka 2010 katika sura 348. Akifungua warsha hiyo leo (16.05.2022) Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi, Bw. Amosi Machilika amesema kuwa lengo la kuandaa daftari la viashiria hatarishi ni kuiwezesha Sekta ya Uvuvi pamoja na wadau wake wanaotekeleza Sera, Mipango, Mikakati na Programu mbalimbali za kisekta kuweza kufikia Malengo yaliyokusudiwa kwa kiwango kikubwa kwa sababu viashiria hatarishi vitakuwa vimewekewa mikakati ya kudhibitiwa kabla ya kutokea na kukwamisha juhudi za Sekta. Machilika amesema kuwa watendaji wa sekta ya uvuvi wanajukumu la kubaini viashiria hatarishi vinavyoikabili sekta, kubuni mikakati Madhubuti ya kudhibiti viashiria hivyo na kuandaa daftari la viashiria hatarishi. Pia amesema kuwa Wakuu wa Idara na Vitengo wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba shughuli za sekta zinatekele...