TANZANIA KUONGEZA NGUVU KUTOKOMEZA SOTOKA YA MBUZI NA KONDOO
Tanzania imeendelea kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (Peste des Petits Ruminants - PPR) kwa kutengeneza Mpango Mkakati wa hadi mwaka 2030, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na nchi jirani katika kudhibiti na hatimaye kutokomeza ugonjwa huo unaoathiri mifugo na maisha ya wafugaji, hatua itakayoiweka Tanzania katika mstari wa mbele barani Afrika katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaodhuru mifugo. Akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kikanda wa PPR uliofanyika leo Septemba 16, 2026 Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa White Sands Resort, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, amesema Mpango huo ni wa kimkakati na ushirikiano wa nchi hizo ni hatua muhimu katika kukabiliana na magonjwa ya mifugo yanayovuka mipaka ya nchi. Mhe. Kamani, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo akimwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema Tanzania imekuwa ikikabiliwa...