MHE. KAMANI AWAITA WAWEKEZAJI KUWEKEZA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

◾Ataka wawekezaji kuzingatia ustawi wa wafanyakazi wao. 

◾Ataka wataalam kutatua changamoto za uhaba wa chakula cha samaki na mifugo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Damas Kamani amewataka wawekezaji nchini kuendelea kuwekeza katika sekta ya mifugo na uvuvi, huku wakizingatia ustawi na usalama wa wafanyakazi wao pamoja na kuhakikisha wanazalisha kwa tija.

Mhe. Kamani ameyasema hayo leo, Septemba 14, 2026, wilayani Magu mkoani Mwanza, wakati wa ziara maalum ya kikazi ya kuwatembelea wawekezaji katika tasnia yaukuzaji viumbemaji, ikiwemo Tangreen Farming Company na M/S ROFI Farming Company Limited, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanyika katika sekta hiyo.

Amesema uwekezaji katika sekta ya mifugo na uvuvi una umuhimu mkubwa katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kutoa ajira na kukuza uchumi, hivyo wawekezaji wanapaswa kuhakikisha wafanyakazi wanapata mazingira salama na stahiki za msingi katika maeneo yao ya kazi.

Aidha, Mhe. Kamani amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na uwekezaji kwa kujifunza ujuzi na teknolojia kutoka kwa wawekezaji, hatua ambayo itawawezesha kuongeza uzalishaji na kujiajiri katika shughuli za mifugo na uvuvi.

Katika hatua nyingine, amewataka wataalam wa serikali kuongeza jitihada za kutatua changamoto ya upatikanaji wa chakula cha samaki na mifugo, ikiwemo kuongeza uzalishaji wa chakula hicho kwa wingi na kwa gharama nafuu, ili kuwawezesha wafugaji na wafugaji wa samaki kuongeza uzalishaji.

Mhe. Kamani amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa tasnia ya ukuzaji viumbemaji, kwa lengo la kuongeza uzalishaji, kukuza ajira na kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi pamoja na kuhakikisha fursa zinazotokana na uwekezaji katika sekta za mifugo na uvuvi zinawanufaisha wananchi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (wa tatu kulia), akikagua miundombinu ya ukuzaji viumbemaji ya Kampuni ya M/S ROFI Farming Company Limited, baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (wa tatu kulia), akikagua miundombinu ya ukuzaji viumbemaji ya Tangreen Farming Company Limited, baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (wa tano kulia), akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Tangreen Farming Company Limited, Bw. Cheng Chang (wa nne kulia) hususu hali ya uzalishaji na changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli ukuzaji viumbemaji, mara baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (wa pili kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S ROFI Farming Company Limited, Bw. Ndungu Liu (wa pili kulia) hususu hali ya uzalishaji na changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli ukuzaji viumbemaji, mara baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026 wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Jubilate Lawuo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, akilisha Samaki kwenye mabwawa ya Kampuni ya M/S ROFI Farming Company Limited, baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (aliyeshika MIC), akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuni ya M/S ROFI Farming Company Limited, baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili, baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani (wa kwanza kulia), akiwatajia namba za Huduma kwa Wateja za Wizara ya Mifugo na Uvuvi Wafanyakazi wa Kampuni ya M/S ROFI Farming Company Limited ili wakihitaji huduma Wizarani iwe rahisi zaidi kuhudumiwa kwa uharaka zaidi, baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili, baada ya kuwasili kwenye Kampuni hiyo ili kujionea shughuli za uzalishaji katika tasnia ya ukuzaji viumbemaji, wakati wa ziara yake ya kikazi ya wilayani Magu Jijini Mwanza, Septemba 14, 2026.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI