Machapisho

WADAU WAHIMIZWA KUFUGA SAMAKI KUKUZA SEKTA YA UVUVI NCHINI

Picha
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza wadau wa sekta ya uvuvi kujikita katika ufugaji wa viumbe maji ili kusaidia kukuza mchango wa sekta ya uvuvi katika Pato la Taifa kutoka asilimia 1.7 walau kufika mpaka asilimia 5 ifikapo mwaka 2025. Prof. Shemdoe alitoa rai hiyo wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa Ukuzaji   Viumbe maji kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 31, 2023. Alisema kuwa hivi sasa wanaandaa kanuni zitakazosaidia kuwa na usimamizi madhubuti wa tasnia ya uvuvi kwa lengo la kuimarisha ukuzaji wa viumbe maji ili kuchangia vyema katika Pato la Taifa. "Tunaandaa kanuni kwa ajili ya ufugaji viumbe maji , kwenye ufugaji wa samaki na mavuvi ya samaki ili kuona   namna tutaweza ndani ya miaka hii miwili   kuchangia   asilimia 5 kwenye pato la taifa," alisema Prof. Shemdoe Aliongeza kuwa kanuni hizo zitakwenda kuboresha namna tasnia ya ukuzaji viumbe maji inasimamiwa na kuwezesha kile kinachozalishwa kiweze kufika kwe...

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

Picha
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame amewataka wataalamwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha wanachukua   takwimu sahihi wakati wa kukusanyataarifa za kitafiti    ili ziweze kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake. Waziri   Shaame ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano   Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha   Oktoba 27, 2023. "Takwimu sahihi kuhusu taarifa za mifugo na uvuvi zitasaidia kutunga sera,   kunyoosha maono, fikra na miongozo ya ilani ya chama cha mapinduzi kuweza kufikia   malengo ya kuwainua wananchi   kupata mafanikio kwa haraka," alisema Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inawategemea sana wataam na hivyo watumie vizuri teknolojia walizonazo ili zikaboreshe tasnia nzima ya ufugaji ili kupata maendeleo. “Wizara ...

WADAU WAKUTANA KUWEKA MIKAKATI KUENDELEZA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Wataalam na wadau wa   sekta ya Mifugo Nchini, wamekutana jijini  Arusha kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza uzalishaji katika sekta hizo ambayo italeta tija  kwa wananchi. Hayo yamesemwa na   Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wazalishaji mifugo na Uvuvi ,Dkt. Jonas  Kizima katika ziara ya kutembelea mbuga ya  Tarangire, ikiwa ni sehemu ya kongamano la siku tatu la kisayansi liloanza Oktoba  26 jijini  Arusha Alisema kuwa  lengo kubwa ni  kupitia machapisho ya kisayansi yaliyoletwa na wadau  ili angalau waweze kutoa matokeo ya tafiti, na kutatua changamoto  katika sekta ya Mifugo na Uvuvi "Katika hizi siku tatu, tumetenga siku moja ya kuja kutembelea mbuga za wanyama nchini, na mwaka huu tumechagua  Tarangire   ili kupata muda wa kufurahi na kujifunza zaidi, Pia tunaunga juhudi za Rais katika kuongeza watalii nchini kupitia Royal  tour na kuongeza pato kupitia utali,"alisema Dkt. Kizima Na...

MIFUGO NA UVUVI YATINGA NUSU FAINALI KIBABE!

Picha
◾ Kukutana na Katiba na Sheria Oktoba 10  Timu ya soka ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetinga hatua ya nusu fainali ya Michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa baada ya kuifumua timu ya bunge kwa magoli 2-1 kwenye mchezo uliochezwa leo Oktoba 08, 2023 uwanja wa Samora mkoani humo. Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi kwa pande zote mbili timu ya Wizara ya Mifugo iliweka kimiani magoli yake kupitia kwa mlinzi wa pembeni Ignatus Mwasa aliyefunga kwa shuti kali la  mpira wa adhabu dakika ya 06 ya mchezo kabla ya timu ya bunge kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Mnubi Kajobi dakika ya 37 na kufanya timu hizo kwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu. Timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa huku ikielekeza mashambulizi ya nguvu upande wa Bunge hali iliyoilazimu timu yote kurudi nyuma kwa ajili ya kuzuia mashambulizi hayo. Mashambulizi hayo makali ya timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi yalizaa matunda katika dakika ya 71 baada ya kupata goli l...

MIFUGO NA UVUVI NAFASI YA 3 BAISKELI WANAUME

Picha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia mshiriki wake Siraji Mohammed imefanikiwa kushika nafasi ya 3 kwenye mashindano ya mbio za baiskeli umbali wa Km.40 yaliyofanyika leo Oktoba 08, 2023 kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa. Siraji ambaye alionesha upinzani wa hali ya juu na kuwa miongoni mwa washiriki 3 wa kwanza walioanza mzunguko wa pili kukamilisha umbali huo huku akitetea nafasi ya 3 aliyoibeba kwenye mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika mkoani Tanga. Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakuwa kibaruani tena leo mchana kwenye hatua ya robo fainali ambapo timu yake ya mpira ya miguu itapepetana na timu ya Bunge huku upande wa mchezo wa kamba wanaume watachuana vikali na timu ya Ikulu.

ULEGA AZITAKA LITA, NARCO KUANDAA VIJANA KUWA WAFANYABIASHARA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amezitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuwa na mkakati wa pamoja wa kuwaandaa vijana kuwa wafanyabiashara katika sekta ya mifugo kupitia programu kielelezo ya BBT Mifugo. Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo wakati akizindua Bodi ya Nne ya Ushauri ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 7, 2023. "Huu ndio uwe mtazamano wetu, kijana anapofundishwa na kumaliza Mafunzo yake pale LITA nyie NARCO muweke utaratibu wa kutenga maeneo kwa ajili ya kuwapa vijana hao ili wajifunze kwa vitendo ufugaji wa kisasa, hatutaki kufundisha watu ili waende kuangaika bali waingie katika biashara ya mifugo na mazao yake," alisema Waziri Ulega  Aidha, aliwataka  LITA kuhakikisha wanakuwa na mkakati wa kuwaunganisha vijana hao na taasisi ...

SERIKALI YADHAMIRIA KUWAINUA VIJANA WA BBT-LIFE KWA KUWATAFUTIA MASOKO YA MIFUGO

Picha
SERIKALI kupitia  Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema kuwa inaendelea na majadiliano  na Wadau wa sekta ya Mifugo nchini  ili kuona namna bora ya kushirikiana na vijana waliopo kwenye Programu ya  BBT  -LIFE katika kunenepesha Mifugo na kuisafirisha kwenye masoko ya nje ya nchi. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi wakati wa  kikao kati ya menejimenti ya sekta mifugo na wadau kuhusu kuwaunga mkono vijana waliopo kwenye programu ya BBT- LIFE , jijini Dodoma, tarehe 06.10.2023. Dkt.Mushi amebainisha kuwa wamekutana na Kampuni za ELIA FOOD na TANCHOICE  Limited za uchakataji nyama  kwa ajili ya  kutengeneza muunganiko wa BBT -LIFE na Soko kubwa la nje ya nchi la uuzaji wa mazao ya Mifugo ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya mifugo kwa vijana wa BBT-LIFE. "Tumefikiria kuwa tukiwapata  wanunuzi wakubwa wa Mifugo programu yetu ya BBT - LIFE itakuwa imefanikiwa katika kuwawezesha vijan...