Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2023

ASILIMIA 90 YA MAZIWA YANAYOZALISHWA NCHINI YAPO NJE YA MFUMO-DKT. MUSHI

Picha
◼️ AWAMWAGIA SIFA ASAS KWA MCHANGO WAO KWENYE JAMII INAYOWAZUNGUKA  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi ameitaka Bodi ya Maziwa nchini kwa kushirikiana na wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa bidhaa hiyo kufanya tathmini ya kina juu ya kiwango cha maziwa yanayozalishwa na kupotea kabla hayajaingia kwenye mfumo rasmi wa uchakataji. Dkt. Mushi amesema hayo Mei 31,2023 wakati akifungua kongamano la wadau wa tasnia ya maziwa lililofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo amebainisha kuwa ni asilimia 10 pekee ya maziwa yanayozalishwa ndio yanayoingia kwenye mfumo rasmi huku asilimia 90 ikiwa haijulikani ilipo. “Kwanza ni lazima tukubali kuwa kiwango cha maziwa cha lita Bil.3.6 kwa mwaka ni kidogo sana ukilinganisha na idadi ya mifugo tuliyonayo lakini pia tungetamani tufike mahali tujitosheleze kwenye matumizi ya maziwa yanayozalishwa hapa nchini kwa sababu kwa  sasa tunatumia maziwa mengi yanayoagizwa kutoka ...

KIKAO KAZI CHA KITAIFA KINACHORATIBU MWONGOZO WA KUENDELEZA UVUVI MDOGO NCHINI CHAFANYIKA MKOANI MOROGORO

Picha
  Mwenyekiti wa kikosi kazi cha kitaifa kinachoratibu Mwongozo wa kuendeleza Uvuvi mdogo Nchini (NTT) Bw. Yahya Mgawe akiongea jambo na  viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) wa mikoa yote Nchini (hawapo pichani) kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa wananwake hao  iliyofanyika katika Ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, iliyoanza leo 30 Mei  hadi 02 Juni 2023. Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi (FRD) Bi. Merisia Mparazo akiongea na wanawake viongozi waliohudhuria warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) (hawapo pichani) Katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (30.05.2023.) Afisa Uvuvi Mkuu, ambaye pia ni Mratibu wa mwongozo wa mradi wa kuendeleza uvuvi mdogo Bi. Lilian Ibengwe akiwasilisha mada kuhusu Mchakato na Mafanikio katika Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi,  kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi...

MAZIWA YASIYO SALAMA NI HATARI KWA MLAJI-SILINDE

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde ameonya kuwa matumizi ya maziwa yasiyo salama huhatarisha maisha ya mlaji kutokana na kutumika kama njia ya kusafirisha  magonjwa ya mifugo kwenda binadamu. Mhe. Silinde amesema hayo kwenye sherehe za ufunguzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Wiki ya unywaji maziwa duniani iliyofanyika Mei 30, 2023 kwenye viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora. “Mwaka huu maadhimisho haya ya Wiki ya unywaji Maziwa kitaifa tumeyaelekeza kwenye kusisitiza matumizi ya maziwa salama kwa sababu kumekuwepo na magonjwa mengi sana yanayosababishwa na maziwa yasiyo salama, mfano ugonjwa wa kutupa mimba ambapo mtu akinywa maziwa yanayotokana na ng’ombe anayeumwa ugonjwa huo naye huanza kuathiriwa  na tatizo hilo hapo hapo” Ameongeza Mhe. Silinde. Mhe. Slinde amewataka Wananchi wote waliopo karibu na mkoa wa Tabora kufika kwenye maonesho hayo ili wapate elimu ya kutosha kuhusu sheria namba 8 ya maziwa ambayo inaanisha kila kitu kuhusu maziwa salama. “Lakini pia...

​VIJANA WANUFAIKA MAFUNZO YA UVUVI KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MIKOPO

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahakikishia vijana walionufaika na mafunzo atamizi ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji na ambao wameshaandaa maandiko ya miradi kuwa watapewa kipaumbele katika kupata mikopo ili waweze kuendeleza miradi yao. Waziri Ulega alitoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo atamizi ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Mwanza Mei 29, 2023. Alisema kuwa Wizara yake inatambua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wawekezaji katika sekta ya uvuvi hivyo kupitia programu hiyo wizara imejipanga kuwasaidia wanufaika wa mafunzo hayo kupata mitaji ya kuanzisha miradi iliyobuniwa kutokana na maandiko waliyowasilisha wizarani. "Juhudi hizi za kutafuta mitaji ni pamoja na ruzuku na mikopo kutoka serikalini, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo. Nipende kusisitiza kuwa uanzishwaji wa vikundi, ushirika au kampuni ni fursa ya kuweza kufikiwa kirahisi na serikali sambamba na kupata fursa za mikopo yenye masharti nafuu ku...

HEKARI 5,520 ZA NARCO ZAKABIDHIWA KWA WANANCHI

Picha
Na. Edward Kondela   Serikali imekabidhi hekari 5,520 za Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kwa wananchi wa wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha Mkoani Pwani ili ziendelezwe kwa shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo za mifugo na kilimo. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (Mb), amebainisha hayo (26.05.2023) katika Ranchi ya Ruvu iliyopo Wilaya ya Kibaha, ambapo amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeridhia kukabidhi hekari 5,520 kwa vijiji 19 vilivyokuwa vimevamia sehemu ya eneo la ranchi na kuwataka wananchi ambao wapo ndani ya mipaka mipya ya Ranchi ya Ruvu kuondoka mara moja. Mhe. Silinde amesema serikali imeridhia kukabidhi hekari hizo baada ya timu iliyoundwa mwaka wa fedha 2019/20 kutoa mapendekezo juu ya vijiji vilivyozunguka Ranchi ya Ruvu ambavyo vilivamia eneo la ranchi hiyo. Ameongeza kuwa kufuatia uamuzi huo wa serikali, amewataka viongozi wa maeneo hayo kupanga mipango bora ya ardhi ili kuondokana na m...

VITUO ATAMIZI VYA MIFUGO VITATUE CHANGAMOTO YA AJIRA KWA VIJANA

Picha
Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) imetakiwa  kuwasimamia vizuri vijana 240 wanaoendelea kupatiwa mafunzo ya unenepeshaji mifugo  katika vituo atamizi 8 chini ya LITA ikiwa ni mpango wa Serikali kusaidia vijana hao kujiajiri na  kujikwamua kiuchumi. Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa LITA kilichofanyika mkoani Arusha Mei 26, 2023. Dkt. Mhina alisema Serikali imeanza kutekeleza mradi huo katika mwaka huu wa fedha baada ya kubaini wataalamu wanaotoka katika vyuo hivyo wanayo nafasi ya kupatiwa ujuzi zaidi ya kuzalisha kupitia vituo atamizi ili watakaporejea mitaani waweze kuwa na uwezo wa kuwekeza zaidi. “Tunatengeneza wataalam ambao ni wawekezaji wao wenyewe watakapoweza kuzalisha ndivyo ambavyo tutaweza kuzalisha malighafi zaidi kwenye viwanda vyetu, kwahiyo hatutarajii wakitoka hapa wakategemee kuajiriwa n...

KIKAO CHA MAPITIO YA RASIMU YA MTAALA WA AFYA YA WANYAMA NA UZALISHAJI CHAFANYIKA MKOANI DODOMA

Picha
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Ugani) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Samwel Mdachi, akifungua kikao cha mapitio ya rasimu ya mtaala wa afya ya wanyama na uzalishaji ili kuingiza masuala ya sumu kuvu kilichofanyika jijini Dodoma kikiwashirikisha washiriki kutoka idara za wizara hiyo sekta ya mifugo pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara. (25.05.2023) Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Asimwe Rweguza akifafanua jambo juu ya rasimu ya mtaala wa afya ya wanyama na uzalishaji pamoja na umuhimu wa malisho ya mifugo wakati wa kikao cha mapitio ya rasimu ya mtaala wa afya ya wanyama na uzalishaji ili kuingiza masuala ya sumu kuvu kilichofanyika jijini Dodoma kikiwashirikisha washiriki kutoka idara za wizara hiyo sekta ya mifugo pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara. (25.05.2023) Afisa Mifugo Msaidizi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Sebastian Shilang...

TUKUTANE TABORA

Picha
 

WIZARA, SUA ZATEKELEZA MAAGIZO YA MHE. RAIS, DKT. SAMIA

Picha
Kufuatia maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ishirikiane na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kuwawezesha vijana kujiajiri yaanza kutekelezwa baada ya pande hizo mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano kuinua sekta za mifugo na Uvuvi. Akiongea muda mfupi baada ya kushuhudia tukio la kusaini makubaliano lililofanyika mkoani Morogoro katika Siku ya Kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine Mei 23, 2023 , Waziri wa Mifugo na Uvuvi alisema tukio hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt Samia aliyotoa katika kilele cha Maadhimisho ya NaneNane yaliyofanyika Mkoani Mbeya Agosti 8, 2022. Alisema kuwa Dkt Samia anataka kuona mabadiliko katika sekta za uzalishaji, hivyo fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji zikitumika vizuri manufaa makubwa yatapatikana ikiwemo kulia kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja. Aidha, Waziri Ulega alimshukuru, Mhe. Rais, Dkt. Samia kwa jitihada zake za kuhamasisha vijana na wanawake k...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

TUKUTANE TABORA

Picha
 

SEKTA YA UVUVI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA MAENDELEO LA KIMATAIFA LA JAPAN (JICA)

Picha
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Sekta ya Uvuvi) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh pamoja na viongozi wengine wa TAFIRI na wizara hiyo, kwenye mazungumzo ya kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Uvuvi kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), ambapo baadhi ya maafisa waandamizi wa shirika hilo hapa nchini walifika katika ofisi za makao makuu ya TAFIRI jijini Dar es Salaam ili kupata taarifa mbalimbali za TAFIRI na maeneo ya kushirikiana. (19.05.2023). Maafisa waandamizi kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) hapa nchini, wakiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na baadhi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mara baada ya maafisa hao kutoka JICA kufika makao makuu ya TAFIRI jijini Dar es Salaam ili kujadili maeneo ya kushirikiana katika Sekta ya Uvuvi na kupata taarifa mbalim...

TUKUTANE TABORA

Picha
 

SERIKALI YAJA NA MPANGO MAALUM WA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI

Picha
Na. Edward Kondela Serikali kuanza kutoa mafunzo maalum ya muda mfupi kwa wafugaji wa samaki kote nchini ili kukuza tasnia hiyo na kuleta tija kwa nchi na wananchi kwa ujumla. Hayo yamebainishwa (19.05.2023) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Sekta ya Uvuvi) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh, mara baada ya wizara hiyo kuingia hati ya makubaliano kupitia Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA) na Chama Kikuu cha Wakuza Viumbe Maji Tanzania (AAT) ili wakala hiyo kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wafuga samaki na watu wanaotaka kuingia katika tasnia hiyo kupitia Mradi wa Kikanda wa Ukuzaji Viumbe Maji (EAC TRUEFISH PROJECT). Prof. Sheikh amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo kwenye sekta za uzalishaji ikiwemo uvuvi kwa kuweka fedha nyingi kwenye ukuzaji viumbe maji hususan ufugaji wa samaki, hivyo kuna haja ya kuweka mafunzo maalum katika ufugaji wa viumbe...