Mwenyekiti wa kikosi kazi cha kitaifa kinachoratibu Mwongozo wa kuendeleza Uvuvi mdogo Nchini (NTT) Bw. Yahya Mgawe akiongea jambo na viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) wa mikoa yote Nchini (hawapo pichani) kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa wananwake hao iliyofanyika katika Ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, iliyoanza leo 30 Mei hadi 02 Juni 2023.
Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi (FRD) Bi. Merisia Mparazo akiongea na wanawake viongozi waliohudhuria warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) (hawapo pichani) Katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, (30.05.2023.)
Afisa Uvuvi Mkuu, ambaye pia ni Mratibu wa mwongozo wa mradi wa kuendeleza uvuvi mdogo Bi. Lilian Ibengwe akiwasilisha mada kuhusu Mchakato na Mafanikio katika Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA), iliyofanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, 30 Mei 2023.
Afisa Uvuvi Mwandamizi ambaye pia ni mratibu wa dawati la jinsia kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Upendo Hamidu akiwasilisha katiba ya "Tanzania Women Fish Workers Association" (TAWFA) ambayo Viongozi hao wataanza kuitumia katika shughuli zote za Uvuvi. Kwenye Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi, katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, 30 Mei 2023.
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Grace Kakama akiwasilisha malengo na Utaratibu wa Warsha ya mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) wa mikoa yote Nchini,(hawapo pichani) mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, 30 Mei 2023.
Katibu wa TAWFA Maji bahari (COWOFO) kutoka Mkoa wa Lindi Wilaya ya Kilwa, Bi. Pili Mkemi ambaye ni mmoja wa wanawake viongozi wanaopata mfunzo ya uongozi na usimamizi kwa viongozi wa TAWFA, Akichangia mada katika majadiliano katika warsha hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, 30 Mei 2023.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi kwa Viongozi wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi Tanzania (TAWFA) wa mikoa yote Nchini, ambayo mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Edema Hotel, Morogoro, 30 Mei 2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni