Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2022

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

WAWEKEZAJI WASIOLIPA KODI, KUFUGA KISASA TUTAWAONDOA-NZUNDA

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda amesema kuwa Serikali itawaondoa kwenye ranchi zake wawekezaji wote wasiofuga kisasa au kulipa kodi ya vitalu walivyokodishwa. Nzunda amesema hayo leo (28.09.2022) mara baada ya kufika na kukagua baadhi ya vitalu vilivyopo kwenye ranchi ya Mkata iliyopo Mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuzitembelea ranchi zilizopo chini ya Kampuni ya ranchi za Taifa (NARCO). “Serikali haitaruhusu ufugaji huu wa kienyeji ndani ya ranchi zake kwa sababu tunataka kuwa na ranchi zinazofanana na ranchi na kwa maneno mengine tungependa kuona wapangaji wetu waliopo kwenye ranchi zetu zote nchini wanakuja na mpango wa kufuga kisasa na kwa kuzingatia mipango ya biashara waliyonayo na kama hamuwezi  kuzingatia mipango hiyo tutaomba mtupishe ili tubaki na wale wenye nia ya kufuga kisasa” Amesisitiza Nzunda. Nzunda ameongeza kuwa kwa muda mrefu Tanzania imekuwa hainufaiki na rasilimali ya mifugo iliyopo n...

PROGRAMU YA SAUTI KULETA MABADILIKO KWENYE SEKTA YA MIFUGO

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa Programu ya Samia Ufugaji kwa Tija (SAUTI) inakwenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye Sekta ya Mifugo.   Waziri Ndaki ameyasema hayo leo (28.09.2022) wakati anazungumza na vijana waliochaguliwa kujiunga kwenye vituo atamizi kwa ajili ya mafunzo ya unenepeshaji mifugo katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Kanda ya Mashariki na Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA) – Buhuri.   Programu ya SAUTI lengo lake ni kuanza kubadilisha fikra za vijana ili waweze kufuga kisasa na kibiashara na kuona kuwa ufugaji unaweza kuwaletea maendeleo makubwa kiuchumi. Aidha, Waziri Ndaki amemshukuru Rais Samia kwa kuiwezesha Wizara kutekeleza Programu hiyo yenye kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mifugo.   Akiwa katika kituo cha TALIRI Kanda ya Mashariki, Waziri Ndaki amewataka watafiti kuhakikisha matokeo ya tafiti wanazozifanya zinawafikia wafugaji ili kuweza kuwabadilisha na kuwafanya waanze kufuga kisasa na kibiashara.   Aidh...

ULEGA ATAKA VIJANA WAWEZESHWE KUJIAJIRI SEKTA YA UVUVI

Picha
Na Mbaraka Kambona, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi una fursa nyingi za kiuchumi hivyo ni muhimu vijana kufundishwa namna ya kutumia fursa hizo kujiajiri ili kujiongezea kipato. Naibu Waziri Ulega alitoa kauli hiyo wakati akiongea na Uongozi wa Shirikisho la Kimataifa linaloshughulika na programu ya uendelezaji wa pwani na uvuvi wa bahari (IUCN) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam Septemba 28, 2022. Alisema kuwa katika ukanda wa pwani wa bahari kuanzia Moa mpaka Msimbati kuna fursa nyingi za ukuzaji viumbe maji ikiwemo ukulima wa mwani, ufugaji majongoo bahari na kaa na tayari kuna jitihada mbalimbali zimeshaanza kuchukuliwa na serikali kuhakikisha fursa hizo za uchumi wa buluu zinawasaidia wananchi hususan vijana na kinamama. “Sasa hivi tuna shilingi bilioni tatu (3) za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajli ya ukulima wa mwani, zitatumika kununulia vifaa vya kulimia  mwani ikiwemo Kamba, Taitai na Mbeg...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

IDARA YA MASOKO TVLA YAKABIDHIWA GARI

Picha
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi amekabidhi Gari jipya aina ya HINO litakalokuwa linatumika kusafirisha Chanjo za Mifugo kutoka kituo cha uzalishaji (TVI) kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani na kuzisambaza kwa wateja maeneo mbalimbali hapa nchini. Akikabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi wa Huduma Saidizi siku ya tarehe 28/09/2022 Makao Makuu ya ofisi za Wakala zilizopo Temeke jijini Dar es salaam alisema kuwa, Wakala imefanikiwa kununua gari la kutunza baridi ambalo ni mahususi kwa ajili ya kusafirishia chanjo kutoka kituo cha uzalishaji chanjo kibaha na kuzisambaza kwa wateja wote nchini.  “Gari hili limenunuliwa kutokana na fedha za ruzuku ya maendeleo, nachukua fursa hii kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutenga bajeti ya maendeleo ambayo imetuwezesha kununua chombo hiki cha usafiri ambacho kitasaidia kuwafikishia wafugaji chanjo kwa wakati.” Alisema Dkt. Bitanyi Dkt Bitanyi aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha ...

WAZIRI NDAKI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI

Picha
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Mashimba Ndaki (katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi ( Kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Evergreen ya nchini Misri, Dkt.Adel Mosalamany (kushoto), akiwa kwenye kikao na Ujumbe toka Kampuni ya Evergreen toka nchini Misri na wataalam wa Uvuvi wakiongozwa na Waziri Mashimba Ndaki, kwa lengo la kujadili fursa zilizopo hapa nchini za  Maeneo ya Kuwekeze kwa masuala ya Uvuvi kwa kampuni ya Evergreen toka nchini Misri ambapo Waziri Mashimba amewakaribisha na kuwahakikishia kupata maeneo wanayohitaji kwa shughuli za Uvuvi.Kikao kimefanyika Mji wa Serikali Mtumba (27.09.2022). Picha ya Pamoja ya Ujumbe wa Kampuni ya Evergreen Kutoka Nchini Misri ikiongozwa na Balozi wa Tanzania toka nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi wa tano toka (kushoto) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh..Mashimba Ndaki wa nne toka kulia,Mwenyekiti wa Kampuni ya Evergreen Dkt.Adel Mosalamany wa tatu toka kulia, Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Ta...

ELIMU YA UDHIBITI WA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA YATOLEWA SHULENI

Picha
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Veterinary iliyopo Manispaa ya Temeke waliokushanyika kwa ajili ya kupata elimu kuhusiana na Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na namna ya Udhibiti wa Ugonjwa huo kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi siku ya tarehe 27/09/2022 Dkt Annette Kitambi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ukaguzi na Ustawi wa Wanyama kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijichi iliyopo Manispaa ya Temeke siku ya tarehe 27/09/2022 alipokwenda kutoa elimu kuhusiana na Maadhimisho ya Udhibiti wa Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa Duniani Meneja wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa yanayoambukizwa na Bioteknolojia kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Jelly S. Chang'a akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Veterinary iliyopo Manispaa ya Temeke kuhusiana na dalili za ugonjwa wa kichaa cha Mbwa, ugongwa unavyosambaa kwenye mwili na madhara yake kwa binadamu siku ya tarehe 27/09/2022 alipo...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

NDAKI AHIMIZA UWEPO WA MFUMO IMARA WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI AFRIKA

Picha
Na Mbaraka Kambona,  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewahimiza Wadau wa Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika (AU) kuhakikisha wanakuwa na mpango madhubuti  wa pamoja wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali hizo ili mchango wake uwe na manufaa makubwa zaidi kwao. Aliyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kurasimisha mpango wa kusimamia rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji  wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 26-28, 2022. Alisema ni wakati sasa nchi za Afrika kuwa na utaratibu wa pamoja wa kuratibu usimamizi wa uendelezaji wa  rasilimali za uvuvi utakaosaidia kulinda ubora, usalama, kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kukuza soko la mazao hayo ndani na nje ya Jumuiya hiyo. "Nimewasisitiza wadau hawa walioshiriki kikao hiki kuwa ni muhimu kutoka na maazimio yatakayosaidia kuratibu vyema uendelezaji wa rasilimali za uvuvi kuliko ilivyo hivi sasa ambap...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI - DODOMA

Picha
 

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

TALIRI YATAKIWA KUTOA MAFUNZO YA MALISHO YA MIFUGO KWA JAMII

Picha
Na. Edward Kondela Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Tixon Nzunda ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), kuongeza uvunaji wa malisho ya mifugo katika vituo vyake vyote nchini ili jamii inayowazunguka iweze kujifunza juu ya ulimaji wa malisho. Katibu Mkuu Nzunda amebainisha hayo (23.09.2022) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika kituo cha TALIRI kilichopo Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma pamoja na kampasi ya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA). Ameongeza kuwa sambamba na jamii inayoishi karibu na vituo vya TALIRI kujifunza juu ya ulimaji wa malisho ya mifugo, jamii hiyo inapaswa pia kujifunza juu ya teknolojia rahisi ya uvunaji wa malisho pamoja na kufahamishwa utaratibu wa ulimaji wa malisho ukiwemo wa undaaji wa mashamba na uvunaji wa mbegu. Ameiasa sekta binafsi kujikita katika biashara ya malisho ya mifugo kwa kuwekeza kwenye vifaa vya uvunaji wa malisho hususan malisho ya asili ambayo kwa sasa ni bias...

SEKTA YA UVUVI YAWEKA SAINI HATI YA USHIRIKIANO WA PROGRAMU YA UKUZAJI VIUMBE MAJI

Picha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) na Mkurugenzi wa programu ya  ukuzaji viumbe maji kutoka Shirika la Gatsby Africa, Bw. Ben Gimson (wa pili kutoka kushoto) wakiweka saini kwenye hati ya ushirikiano kati ya Shirika hilo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) yenye lengo la  kuweka mazingira mazuri ya kisera kwa  kuwezesha ukuaji wa tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji, kutoa msaada wa kiufundi kwa wafugaji samaki kibiashara ili kuongeza uzalishaji na tija na kuwezesha mpango wa matumizi bora ya Ziwa Victoria katika muktadha wa ufugaji samaki kwa vizimba. Septemba 23,2022 Jijini dar es salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Programu ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Shirika la Gatsby Africa, Bw. Ben Gimson (wa pili kutoka kushoto) na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kuweka Saini kwenye hati ya ushirikiano baina ya Shi...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

WAZIRI NDAKI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA

Picha
  Waziri  wa Mifugo na Uvuvi Mh.Mashimba Ndaki akiwa kwenye kikao na Ujumbe toka Banki ya Dunia ofisini kwake na baadhi ya watendaji wa Wizara kwa lengo la kujadili Maeneo ya takayofadhiliwa na Banki ya Dunia  Baadhi ya Maeneo ni pamoja na ,Ufadhili katika uanzishwaji wa vituo Atamizi vya Mifugo na Ukuzaji viumbe Maji (Uvuvi), Kuiwezesha NARCO , Masuala ya Uhimilishaji na Utafiti Katika Sekta za Mfugo na Uvuvi.Ambapo Mheshimiwa Waziri aliwashukuru na kuahidi yuko tayari kushirikiana nao katika maeneo yaliyoinishwa    ya ufadhili wa Banki ya Dunia.Kikao kimefanyika ofisi za Wizara NBC Dodoma (23.09.2023) Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Katikati Mh.Mashimba Ndaki na Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Tixon Nzunda wa kwanza kushoto, na Mkuu wa msafara wa Banki ya Dunia Holger  kray kushoto kwa waziri Mashimba Ndaki,na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt.Hamisi Nukuli wa kwanza kulia (23.09.2023).

ULEGA AMALIZA MKWAMO WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA BUKASIGA

Picha
Na Martha Mbena. Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amemaliza mkwamo wa utekelezaji wa mradi wa ukaushaji dagaa wa chama cha Ushirika cha BUKASIGA uliopo katika kisiwa cha Ghana, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe. Mhe. Ulega alifanikiwa kuumaliza mkwamo huo wakati alipokuwa akiendesha kikao kazi cha kujadiliana namna bora ya kukubaliana kati ya chama cha Ushirika cha BUKASIGA, Sokoine University Graduates Entreprenuers Cooperative" (SUGECO) na Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano, Jengo la Nbc,Dodoma. 22 Septemba 2022. Mhe. Ulega amesema pande zote mbili wamefikia mahali pazuri na mwanga umeonekana na watu wamekubaliana kule ambapo wamepakusudia. "Nawapongeza sana kwasababu washirika hawa wameitika wito wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwakuweza kufanya kazi kwa bidii kuweza kujenga uchumi wa nchi yetu" Amesema Mhe. Ulega. Pia Mhe. Ulega ameagiza chama cha ushirika cha BUKASIGA  na watu wa SUGECO Kuand...