Nav bar

Ijumaa, 30 Septemba 2022

SEKTA YA UVUVI YAWEKA SAINI HATI YA USHIRIKIANO WA PROGRAMU YA UKUZAJI VIUMBE MAJI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) na Mkurugenzi wa programu ya  ukuzaji viumbe maji kutoka Shirika la Gatsby Africa, Bw. Ben Gimson (wa pili kutoka kushoto) wakiweka saini kwenye hati ya ushirikiano kati ya Shirika hilo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) yenye lengo la  kuweka mazingira mazuri ya kisera kwa  kuwezesha ukuaji wa tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji, kutoa msaada wa kiufundi kwa wafugaji samaki kibiashara ili kuongeza uzalishaji na tija na kuwezesha mpango wa matumizi bora ya Ziwa Victoria katika muktadha wa ufugaji samaki kwa vizimba. Septemba 23,2022 Jijini dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Programu ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Shirika la Gatsby Africa, Bw. Ben Gimson (wa pili kutoka kushoto) na watendaji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kuweka Saini kwenye hati ya ushirikiano baina ya Shirika hilo na Wizara, lengo likiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kisera kwa  kuwezesha ukuaji wa tasnia ya Ukuzaji Viumbe Maji, kutoa msaada wa kiufundi kwa wafugaji samaki kibiashara ili kuongeza uzalishaji na tija na kuwezesha mpango wa matumizi bora ya Ziwa Victoria katika muktadha wa ufugaji samaki kwa vizimba. Septemba 23,2022 Jijini dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni