Nav bar

Ijumaa, 30 Septemba 2022

WAZIRI NDAKI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MISRI

 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Mashimba Ndaki (katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi ( Kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Evergreen ya nchini Misri, Dkt.Adel Mosalamany (kushoto), akiwa kwenye kikao na Ujumbe toka Kampuni ya Evergreen toka nchini Misri na wataalam wa Uvuvi wakiongozwa na Waziri Mashimba Ndaki, kwa lengo la kujadili fursa zilizopo hapa nchini za  Maeneo ya Kuwekeze kwa masuala ya Uvuvi kwa kampuni ya Evergreen toka nchini Misri ambapo Waziri Mashimba amewakaribisha na kuwahakikishia kupata maeneo wanayohitaji kwa shughuli za Uvuvi.Kikao kimefanyika Mji wa Serikali Mtumba (27.09.2022).

Picha ya Pamoja ya Ujumbe wa Kampuni ya Evergreen Kutoka Nchini Misri ikiongozwa na Balozi wa Tanzania toka nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi wa tano toka (kushoto) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh..Mashimba Ndaki wa nne toka kulia,Mwenyekiti wa Kampuni ya Evergreen Dkt.Adel Mosalamany wa tatu toka kulia, Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, wa kwanza toka kushoto,mara baada ya Kikao cha Wajumbe hao na wataalam wa Uvuvi wakiongozwa na Waziri Mashimba Ndaki cha Kubaini fursa za  maeneo ya kuwekeza katika Uvuvi kwa Kampuni ya Evergreen toka nchini Misri.Picha imechuliwa katika Ofisi  za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, (27.09.2022)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni