Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Veterinary iliyopo Manispaa ya Temeke waliokushanyika kwa ajili ya kupata elimu kuhusiana na Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na namna ya Udhibiti wa Ugonjwa huo kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi siku ya tarehe 27/09/2022
Dkt Annette Kitambi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ukaguzi na Ustawi wa Wanyama kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijichi iliyopo Manispaa ya Temeke siku ya tarehe 27/09/2022 alipokwenda kutoa elimu kuhusiana na Maadhimisho ya Udhibiti wa Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa Duniani
Meneja wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa yanayoambukizwa na Bioteknolojia kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Jelly S. Chang'a akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Veterinary iliyopo Manispaa ya Temeke kuhusiana na dalili za ugonjwa wa kichaa cha Mbwa, ugongwa unavyosambaa kwenye mwili na madhara yake kwa binadamu siku ya tarehe 27/09/2022 alipokwenda kutoa elimu ya Maadhimisho ya Udhibiti wa Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa Duniani
Daktari Muandamizi kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya Mifugo Kanda ya mashariki ZVC-TEMEKE Dkt Abdul S. Kyarumbika akitoa elimu ya kujikinga na kuchukua tahadhari mara baada ya kung’atwa na Mbwa mwenye kichaa kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Veterinary siku ya tarehe 27/09/2022 iliyopo Manispaa ya Temeke alipokwenda kutoa elimu kuhusiana na Maadhimisho ya Udhibiti wa Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa Duniani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni