Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2021

MATEMBEZI YA HIARI NA UPANDAJI MITI ILIYOFANYIKA KATIKA ENEO LA MEDELI TAREHE 29.05.2021

Picha
*Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye Matembezi ya Hiari - Mazingira Walk kuanzia viwanja vya Bunge kuelekea eneo la Medeli kwa ajili ya zoezi la Upandaji Miti lililoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Selemani Jafo leo tarehe (29.05.2021) Jiji Dodoma * * Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (mwenye T-shirt nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi kabla ya kuanza zoezi la Upandaji miti katika eneo la Medeli lillozinduliwa leo tarehe (29.05.2021)Jiji Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo. Wengine ni Afisa Uvuvi Bw. Makorwa Hamadi (wa kwanza kushoto), Mkuu wa kitengo cha Mazingira (Uvuvi) Bw.Melton Kalinga (wa kwanza kulia) akifutiwa  na Afisa Uvuvi Mkuu Bi. Magreth Dominick Gg

HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHESHIMIWA MASHIMBA MASHAURI NDAKI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA 2021/2022

HOTUBA YA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHESHIMIWA MASHIMBA MASHAURI NDAKI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KWA MWAKA 2021/2022  

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2021-2022

Picha
 

MWALIKO WA KIKAO

Picha
 

TUTAENDELEA KUBORESHA MASHAMBA YA SERIKALI – ULEGA.

Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Abdalla Ulega amesema Wizara hiyo ina mkakati wa miaka mitatu (2020/2021 – 2022/2023) ambao umelenga kuendeleza mashamba kwa kuongeza ng’ombe wazazi na kuimarisha huduma za uhimilishaji ili kupata ngombe bora na wenye tija. Ulega aliyasema hayo  bungeni Mei 24, 2021 wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Mhe. Festo Sanga ambaye alitaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kuendeleza Shamba la Mifugo la Kitulo. Mhe. Ulega alisema kuwa katika kutekeleza Mkakati huo Wizara kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022 imenunua madume matano (5) ya ng’ombe wazazi kutoka shamba la Shafa Farm lililopo mkoani Iringa, kilo 400 za mbegu za malisho kutoka Marekani na nyingine 100 kutoka Kenya kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa malisho.   Alisema, shughuli nyingine ni uhimilishaji ambapo ng’ombe 135 wamehimilishwa na ununuzi wa tenki la kupoozea maziwa lenye ujazo wa lita 3,000 ambapo utaratibu wa manunuzi unakamilishwa. “Shamba la Kitulo linahitaji u...

SERIKALI YASISITIZA UPATIKANAJI WA TAARIFA SAHIHI ZA UVUVI MDOGO

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesisitiza upatikanaji wa taarifa sahihi za uvuvi mdogo nchini  kwa kuangaza taarifa za wavuvi wadogo zilizofichika ili ziweze kutumika kwa mipango ya maendeleo endelevu kwa lengo la kukuza Uchumi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya uvuvi ya kupitia matokeo ya utafiti wa mchango wa Uvuvi mdogo iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE) Dkt. Erastus Mosha mjini Morogoro (21.5.2021). Akisoma hotuba hiyo, Mkurugenzi amewakumbusha wadau kuwa Uvuvi ni sayansi, hivyo usimamizi wa rasilimali hiyo ni muhimu na unahitaji taarifa za kutosha za kitafiti ili kufikia malengo ya kuwa na Uvuvi endelevu nchini. Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya Uvuvi kwa muda mrefu kuwa ni kukosekana kwa taarifa sahihi za mavuvi, zana haramu, idadi ya wavuvi, vyombo vya Uvuvi na nying...

WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA DAWA ZA MIFUGO WATAKIWA KUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI

Picha
Wauzaji na wasambazaji wa madawa ya mifugo wametakiwa kuzingatia utaratibu ambao umewekwa na Serikali kupitia Baraza la Veterinari Tanzania ili kutoa huduma stahiki kwa wafugaji. Hayo yalisemwa na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania, Dkt. Bedan Masuruli  wakati wa kikao na wauzaji na wasambazaji wa dawa kilichojadili kuhusu changamoto zinazohusu tasnia ya Mifugo kwenye uuzaji na udhibiti wa madawa  kilichofanyika  Jijini Dar es Salaam Mei 19, 2021. Dkt. Masuruli alisema kuwa bado lipo tatizo kwa baadhi ya wauzaji na wasambazaji wa madawa hayo kutozingatia taratibu ambazo zimewekwa na hivyo kusababisha madhara kwa wafugaji kwa kutopata huduma stahiki. Aliongeza kuwa wauzaji na wasambazaji wa madawa hayo wanatakiwa kufuata na kuzingatia utaratibu uliowekwa kwa kuhakikisha madawa yote ya mifugo yanauzwa sehemu ambayo ni sahihi na imesajiliwa na kutambulika na Baraza la Veterinari Tanzania. Aidha, Dkt. Masuruli aliwahimiza wamiliki hao kuwatumia wataalam wa mifug...

SERIKALI KUWEKA UTARATIBU WA KUVUA KAMBAMITI*

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka utaratibu wa kuvua kambamiti kwa wavuvi wakubwa na wadogo ili kufanya kambamiti waweze kuzaliana na kukua. Hayo yamebainishwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Twaha Ally Mpembenwe, ambaye alitaka kufahamu ni lini serikali itatoa uamuzi wa kuwaruhusu wavuvi wa kambamiti kuvua kuanzia mwezi Desemba hadi Julai kila Mwaka. Alisema, utaratibu huo wa kuvua kambamiti umewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo unaruhusiwa kufanyika kuanzia mwezi Machi hadi Septemba kila mwaka kwa ukanda wa Kaskazini unaohusisha Wilaya za Bagamoyo, Pangani na Chalinze na kuanzia mwezi Aprili hadi Agosti kila mwaka kwa Ukanda wa Kusini unaohusisha Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Kilwa. Aliongezea kuwa, kipindi kilichobaki kimeachwa ili kambamiti waweze kuzaliana na kukua. Maamuzi haya yamefanyika baada ya taarifa za utafiti wa kisayansi na kuzingatia uendel...

WAWEKEZAJI WATAKIWA KUGEUKIA FURSA YA KILIMO CHA MBEGU ZA MALISHO YA MIFUGO

Picha
Serikali imewataka wadau wa uwekezaji nchini kugeukia Sekta ya Mifugo hasa katika kutumia fursa ya changamoto ya uhaba wa mbegu za malisho ambayo mahitaji yake ni zaidi ya tani milioni 7 kulinganisha uzalishaji wa sasa wa tani 127 pekee. Rai hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akifungua warsha maalum ya wadau wa uzalishaji mbegu za malisho hapa nchini  Mkoani Morogoro 12, Mei 2021. Alisema kuwa takwimu zinaonyesha kiwango cha uzalishaji wa mbegu ni mdogo ukilinganisha na mahitaji yake na kwamba kama wawekezaji wakigeuza changamoto hiyo kuwa fursa inasadia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji. “Mahitaji ya mbegu za malisho Tanzania ni tani milioni 7 lakini kiwango cha  mbegu kilichozalishwa kwa mwaka 2019/20 ni tani 127 maana yake ni kwamba kuna uhaba mkubwa sana ivyo changamoto hiyo tuichukulie kama fursa ya uwekezaji katika sekta hiyo” alisema Prof Gabriel. Kadharika alisema Serikali kupitia Wiz...

KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC) WENYE DHAMANA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha makatibu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya  kilimo, mifugo na uvuvi. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Andrew Massawe na Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa kwenye maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa SADC utakaofanyika Tarehe 07 Mei 2021. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Mkutano huo unafanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa na nchi wanachama wa SADC. (05.05.2021) Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha makatibu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya  kilimo, mifugo na uvuvi, kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa SADC utakaofanyika Tarehe 07 Mei 2021. ...

WAVUVI WAHIMIZWA KUJIUNGA KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA

Serikali imeendelea kuhamasisha uanzishwaji na uimarishaji wa vikundi na vyama vya ushirika vya msingi vya  wavuvi  wadogo kwa lengo la kuwapatia mtaji, ujuzi, vifaa pamoja na dhana za uvuvi katika maeneo ya mwambao wa bahari ya hindi , maziwa, mabwawa na mito ili kuzalisha ajira na kipato.  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, Mhe. Eng. Stella Manyanya   ambaye alitaka kufahamu mikakati ya Serikali katika kuhakikisha mikopo inatolewa kwa mtu mmoja mmoja aliye tayari, kuliko kutoa kupitia vikundi jambo ambalo linachelewesha ukuaji wa sekta ya uvuvi. Mhe. Ulega alisema kuwa katika kutekeleza ilani  kwa mwaka wa fedha 2020/2021 serikali iliadhimia kuhamasisha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili kuwa na sauti ya pamoja ikiwa ni rahisi kutatua changamoto zinazowakabili kwa pamoja na kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za uvu...

WAKAGUZI WA NGOZI WATAKIWA KUHAKIKISHA UZALISHAJI WA NGOZI BORA*

Picha
    Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa mafunzo na kuwakabidhi majukumu wakaguzi wa ngozi 33, kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria ili kuhakikisha ngozi inayozalishwa nchini inakuwa bora. Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.  Gabriel Bura, aliyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa ngozi yaliyofanyika jijini Mwanza Mei 5, 2021. Alisema, wakaguzi wa ngozi waliopatiwa mafunzo kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu wanatakiwa kuongeza usimamizi wa sheria ya biashara ya ngozi. “Hii ni kutokana  na kati ya  asilimia 100 ya ngozi zinazopelekwa viwandani,  asilimia 10  ndizo zinafaa kusindikwa  na kutengenezea bidhaa huku asilimia 90 hazifai kutokana na kukosa ubora unaotakiwa, ambapo jambo hilo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara na wenye viwanda.” Alisema Aliongeza kuwa watahakikisha uzalishaji wa ngozi unakuw...

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Picha
 

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

Picha
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),  Prof. Hezron Nonga, ametoa wito kwa  watumishi wa umma kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua afya zao kama ambavyo muongozo wa kudhibiti virusi vya ukimwi (VVU), Ukimwi na magonjwa sugu yasiyo ambukiza mahala pa kazi unavyowataka.   Prof. Nonga, aliyasema hayo  wakati akifungua mafunzo pamoja na upimaji wa afya kwa watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaliyofanyika Jijini Dodoma Aprili 30, 2021.   Alisema kuwa upimaji wa afya kwa watumishi wa umma kwa mujibu wa muongozo huo wa mwaka 2014 ni jambo la lazima siyo hiyari.   “Kupima afya ni jambo la lazima na muhimu sana kwa mtumishi kwani itasaidia hata kuongeza tija katika taasisi baada ya kutambua afya yake” amesema Prof.Nonga.   Aidha amesema kuwa kwa kutambua afya za wafanyakazi kutamwezesha  mwajiri kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa jukumu mbalimbali.   “Kama mtumishi atakuwa na afya njema basi ...