Wajumbe kutoka Tanzania wakiwa katika kikao cha makatibu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya kilimo, mifugo na uvuvi, kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa SADC utakaofanyika Tarehe 07 Mei 2021. Ujumbe wa Tanzania umehudhuria mkutano huo kwenye ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Mkutano huo unafanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa na nchi wanachama wa SADC. (05.05.2021)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha makatibu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya kilimo, mifugo na uvuvi, akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Andrew Massawe (katikati) na Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa SADC utakaofanyika Tarehe 07 Mei 2021. Ujumbe wa Tanzania umehudhuria mkutano huo kwenye ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Mkutano huo unafanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa na nchi wanachama wa SADC. (05.05.2021)
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi)
Bw. Adam Mwaigoga (katikati), Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Bw. Didas Mtambalike (kulia) na Mkurugezi wa Idara ya Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Obadiah Nyagiru wakibadilishana mawazo kabla ya
kuanza kwa kikao cha maandalizi ya mkutano wa mawaziri wa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wenye dhamana ya kilimo, mifugo na uvuvi, utakaofanyika Tarehe
07 Mei 2021. Ujumbe wa Tanzania umehudhuria mkutano huo kwenye ukumbi wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki katika Mji wa Serikali
Mtumba jijini Dodoma. Mkutano huo unafanyika kwa njia ya video na kuhudhuriwa
na nchi wanachama wa SADC. (05.05.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni