Machapisho

TASFAM YATAJWA KUONGEZA WIGO, KUKUZA SEKTA YA UVUVI

Picha
 Na. Edward Kondela ‎Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema uvuvi wa bahari kuu, ukuzaji viumbe maji, mafunzo na utafiti ni mambo muhimu katika kukuza Sekta ya Uvuvi nchini. ‎Mhe. Balozi Dkt. Kakurwa amebainisha hayo leo (05.11.2026) jijini Dodoma, alipokutana na watekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kutoka katika taasisi na idara zinazoshughulika na Sekta ya Uvuvi zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. ‎Amesema mafunzo na utafiti yanaenda sambamba na uwepo wa maabara yenye ubora na usalama kwa ajili ya sampuli za bidhaa za uvuvi ili kuleta matokeo chanya. ‎Ameongeza kuwa ni muhimu kutatua kwa haraka changamoto zozote zitakazokuwa zinajitokeza ili kutochelewesha baadhi ya shughuli katika utekelezaji wa mradi. ‎Awali kwenye kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh, amesema atahakikisha mradi wa TASFAM, unaleta matokeo chanya yaliyokusudiwa, kati...

BUNGE LAPITISHWA MRADI WA MAGEUZI TASNIA YA MAZIWA, MABADILIKO YA TABIANCHI

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani ameiongoza Wizara yake kulipitisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi kwenye semina fupi iliyofanyika Novemba 05,2026 Bungeni jijini Dodoma. Akizungumza mara baada ya kujengewa uelewa kuhusu mradi huo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Mariam Ditopite ametoa wito kwa wabunge kuwa mabalozi wa mradi huo kwenye maeneo yao unakotekelezwa ili kusaidia wafugaji kubadilika na kurasimisha biashara ya maziwa nchini. “Tumeona mfumo mzima wa uuzaji wa maziwa yetu mengi yanaenda kwenye masoko yasiyo rasmi hivyo kwa utaratibu huu wa kujenga vituo vya kukusanyia maziwa na vifaa vya kisasa vya kusambazia maziwa naamini tutakuwa tumetibu changamoto hiyo” Amesema Mhe. Ditopile Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani mbali na kulishukuru Bunge kwa kuwapa fursa ya kuwapitisha kwenye mradi huo ameahidi kufanyia kaz...

MAFUNZO YA TDB YAIBUA UWEZO MPYA KWA WADAU WA MAZIWA MUFINDI

Picha
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), imeendelea kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, kwa kuwapatia elimu na ujuzi wa vitendo kuhusu ubora na usalama wa maziwa. Mafunzo hayo yaliyofanyika Novemba 4, 2026, yalilenga kuwawezesha wadau kutumia kanuni bora za usafi katika uzalishaji na ushughulikiaji wa maziwa, pamoja na kujifunza mbinu rahisi za kupima na kuhakiki ubora wake. Afisa  Mtekinolojia wa Chakula kutoka TDB Bw. Israel Mwingira aliwaongoza washiriki katika mafunzo ya vitendo kuhusu namna ya kutambua ubora wa maziwa na kuzingatia taratibu za usalama katika shughuli zao za kila siku. Katika sehemu nyingine ya mafunzo, Mwanasheria wa TDB Wakili Msomi Haruna Maarufu alitoa ufafanuzi kuhusu sheria inayoipa Bodi mamlaka ya kusimamia na kudhibiti Tasnia ya Maziwa nchini. Aliwakumbusha washiriki kuhusu wajibu wa kisheria wa kujisajili ...

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUMALIZA MGOGORO WA SHAMBA LA TVLA MIVUMONI

Picha
TAKUKURU yaagizwa kuchunguza ugawaji wa ardhi, shughuli za ujenzi na kilimo zasitishwa. Na Daudi Nyingo – Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, ameagiza kuhakikiwa kwa mipaka na kusitishwa kwa shughuli za uendelezaji katika eneo la mgogoro wa muda mrefu wa uvamizi wa Shamba la Serikali la Utafiti na Mifugo Mivumoni, linalosimamiwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ili kutatua mgogoro wa muda mrefu wa uvamizi unaohusisha wananchi wa Kijiji cha Kigurusimba, Wilaya ya Pangani. Akizungumza na wananchi kijijini hapo Novemba 3, 2026 amesema ndege nyuki (drone) zitatumika kupata picha za hali ya eneo kabla ya wataalamu kuweka alama za mipaka na kubainisha majengo yaliyo ndani ya shamba na pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza namna maeneo hayo yalivyogawiwa, huku TVLA ikithibitisha kuachia hekta 1,271 kati ya hekta 5,320 kwa Serikali ya Kijiji kwa ajili ya kuwagawia wananchi. “...

NJOMBE YAWEKA MSISITIZO KWENYE MAZIWA SALAMA KUPITIA MAFUNZO YA WADAU WA TASNIA

Picha
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbinu bora za uzalishaji na ushughulikiaji wa maziwa kwa kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Mafunzo hayo yaliyofanyika Novemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, yalilenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu masuala ya ubora na usalama wa maziwa katika hatua zote za uzalishaji, ukusanyaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji. Timu ya wataalamu kutoka TDB iliongozwa na Bw. Israel Mwingira, Afisa Mtekinolojia wa Chakula, ambaye aliratibu utoaji wa elimu kwa wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia taratibu bora za ushughulikiaji wa maziwa ili kuzuia uchafuzi na kuhakikisha yanakidhi viwango vya ubora na usalama. Kupitia mafunzo hayo, TDB na C-SDTP zinaendelea kuimarisha ujuzi wa wadau na kuhamasisha uwajibikaji katika mnyororo wa thamani wa maziwa, kwa lengo la kuonge...

TDB NA C-SDTP WAENDELEA KUJENGEA UWEZO WADAU WA TASNIA YA MAZIWA SIHA

Picha
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Siha, imeendelea kutoa elimu na kujenga uwezo wa wadau wa tasnia ya maziwa ili kuboresha uzalishaji, ukusanyaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji wa maziwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama. Mafunzo hayo yaliyofanyika Oktoba 31, 2026, katika Ukumbi wa Jimboni, Sanya Juu, yalilenga kuwawezesha wadau kuelewa taratibu, kanuni na matakwa ya kisheria yanayosimamia shughuli za tasnia ya maziwa nchini. Akizungumza kwa niaba ya Msajili wa TDB, Bi. Neema Moshi, aliwahimiza wadau kujisajili Bodi ya Maziwa kwa mujibu wa Sheria ya Tasnia ya Maziwa, Sehemu ya 17(1), inayomtaka kila anayejihusisha na biashara ya maziwa na bidhaa zake kusajiliwa.  Alieleza kuwa usajili unawezesha Bodi kuwatambua na kuwasimamia wadau kupitia ukaguzi, elimu na ushauri wa kitaalamu ili kuhakikisha maziwa yanazalishwa na kushughulikiwa katika mazin...

WAZAZI LUGANGA NA POMERINI WAUNGA MKONO MPANGO WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI KUBORESHA LISHE YA WANAFUNZI

Picha
Wazazi na Kamati za Shule za Msingi Luganga na Pomerini, zilizopo Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa, wameonesha mwitikio mkubwa na kuunga mkono juhudi za kuanzisha Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni, unaolenga kuboresha lishe, afya na ukuaji wa wanafunzi.                         Msimamo huo umejitokeza katika vikao vilivyofanyika kwa nyakati tofauti Novemba 03, 2026, vilivyolenga kujadili namna ya kushirikiana katika kuanzisha na kutekeleza mpango huo shuleni. Akizungumza katika vikao hivyo, Meneja Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Joseph Semu, alieleza umuhimu wa kuwa na Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni, akibainisha kuwa maeneo mbalimbali ambako mpango huo umetekelezwa yameonesha matokeo chanya katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ustawi wa wanafunzi.  Alisisitiza kuwa maziwa ni sehemu muhimu ya lishe bora, hivyo ushiriki wa wazazi na jamii ni nguzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata fursa ya ku...