NJOMBE YAWEKA MSISITIZO KWENYE MAZIWA SALAMA KUPITIA MAFUNZO YA WADAU WA TASNIA

Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbinu bora za uzalishaji na ushughulikiaji wa maziwa kwa kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

Mafunzo hayo yaliyofanyika Novemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, yalilenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu masuala ya ubora na usalama wa maziwa katika hatua zote za uzalishaji, ukusanyaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji.

Timu ya wataalamu kutoka TDB iliongozwa na Bw. Israel Mwingira, Afisa Mtekinolojia wa Chakula, ambaye aliratibu utoaji wa elimu kwa wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia taratibu bora za ushughulikiaji wa maziwa ili kuzuia uchafuzi na kuhakikisha yanakidhi viwango vya ubora na usalama.

Kupitia mafunzo hayo, TDB na C-SDTP zinaendelea kuimarisha ujuzi wa wadau na kuhamasisha uwajibikaji katika mnyororo wa thamani wa maziwa, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa maziwa salama na bora, kulinda afya za walaji na kuchochea maendeleo ya Tasnia ya Maziwa nchini.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI