TALIRI YATAKIWA KUFANYA TAFITI ZITAKAZOLETA TIJA SEKTA YA MIFUGO.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), kufanya tafiti zitakazo lisaidia taifa kupiga hatua kupitia sekta ya mifugo. Prof. Ole Gabriel, aliyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya jiji Mkoani Dodoma Aprili 23, 2021. Akizungumza na Wajumbe wa baraza hilo Prof. Ole Gabriel alisema kuwa, hakuna Taasisi nyingine ambayo Wizara hiyo inaweza kuitegemea katika suala la utafiti zaidi ya TALIRI, hivyo ni lazima ifanye tafiti zitakazo boresha sekta ya mifugo nchini na kuchangia pato la taifa. “Tusibakie kujisifu tuu kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa idadi kubwa ya mifugo lazima tujisifie kwa namna tutavyoweza kutumia sekta hii kukuza uchumi wa taifa” alisema Prof. Ole Gabriel Alisema kuwa tafiti ndizo zinaweza kulisadia taifa kutoka h...