Na Mbaraka Kambona,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba
Ndaki amewataka watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujiepusha na vitendo
vya rushwa huku akionya kuwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo
hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Ndaki aliyasema hayo wakati akifungua
Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo
uliofanyika jijini Dodoma Aprili 20, 2021.
Akizungumza na Wajumbe wa baraza hilo,
Ndaki aliwataka watumishi hao kuzingatia uadilifu na uwajibikaji katika
utekelezaji wa shughuli za serikali huku akisema siyo vyema kwa mtumishi wa
umma kutajwatajwa kuhusika na matukio maovu yanayoharibu taswira ya serikali.
"Niwaombe watumishi wote mjiepusha
na vitendo vinavyokwenda kinyume cha Sheria za nchi na taratibu za kazi, haipendezi
kuona mtumishi wa umma anatajwatajwa kwenye kashfa za rushwa, hili siyo jambo
jema hata kidogo, epukeni rushwa,”alisema Ndaki
Aliongeza kuwa watumishi ni muhimu
wakaheshimiana na kuzingatia nidhamu ya kazi, wajiepushe na vitendo vya ubabe
na kudharauliana huku akisema kuwa kila mtu katika kazi ana umuhimu wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza
hilo, Prof. Elisante Ole Gabriel alimuahidi Waziri Ndaki kuwa wamepokea
maelekezo yake na watahakikisha wanayasimamia vizuri ili kuongeza tija na ufanisi
katika kazi.
Prof. Ole Gabriel aliongeza kuwa kupitia baraza
hilo wataendelea kuboresha bajeti ya sekta ya mifugo ili waweze kuwanyanyua
wafugaji waweze kufanya ufugaji wa
kisasa na kuachana na ufugaji wa mazoea.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akiongea na Wajumbe wa Baraza
la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) wakati akifungua Mkutano
wa baraza hilo ambapo aliwasisitiza Watumishi wa Wizara kuzingatia Uadilifu,
nidhamu na kujiepusha na vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mkutano huo ulifanyika jijini Dodoma. (20.04.2021)
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiongea na Wajumbe wa baraza
hilo wakati akitoa neno la shukrani kwa (Mgeni rasmi), Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mashimba Ndaki (kushoto) katika
Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)
uliofanyika jijini Dodoma. (20.04.2021)
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) wakifuatilia
matukio katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo) uliofanyika jijini Dodoma (20.04.2021)
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Flaxed Mushi
(kulia) akifuatilia majadiliano katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) uliofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi, Rasilimali Watu, Josephine Temihango. (20.04.2021)
Mhasibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Veronica Kishala
(kulia) akifurahia jambo wakati akiongea na Afisa Usafirishaji, Kennedy Laizer
walipokutana katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Mifugo) uliofanyika jijini Dodoma. (20.04.2021)
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi, Idara
ya Sera na Mipango, Amos Zephania walipokutana katika Mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) uliofanyika jijini Dodoma. (20.04.2021)
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) wakimsikiliza Mgeni rasmi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mashimba Ndaki wakati alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo
uliofanyika jijini Dodoma. (20.04.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni