Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekutana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, ikiwemo Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) – Uvuvi, utoaji wa boti za kisasa za uvuvi pamoja na kuanzisha utaratibu wa Mfuko wa Mikopo Endelevu utakaotokana na miradi hiyo.
Kikao hicho ambacho kimefanyika leo Novemba 11, 2026 Jijini Dodoma kimejadili namna bora ya kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwa wanufaika na kuchochea maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini.
Aidha, mjadala umejikita katika kuweka utaratibu utakaowezesha fedha zitakazorejeshwa kupitia miradi hiyo kuendelea kutumika kuwafikia wanufaika wengine kupitia Mfuko wa Mikopo Endelevu.
Kikao hicho kimefanyika chini ya uongozi wa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (DRTE), Ndg. Samwel Mdachi, ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi (DRTE), Ndg. Samwel Mdachi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kikao, akitoa neno la ufunguzi, katika kikao kilichojumuisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi (DRTE), Ndg. Samwel Mdachi (katikati), akijibu hoja mbalimbali za wajumbe, katika kikao kilichojumuisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TADB pamoja na FETA kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo ya Mifugo na Uvuvi Nchini, Bi. Emelda Adam kulia ni Afisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ambakisye Simtoe.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dkt. Semvua Mzighani (kulia), akichangia hoja, katika kikao kilichojumuisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na FETA kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma.
Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi, akichangia hoja, katika kikao kilichojumuisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma.
Meneja Usimamizi wa Miradi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bi. Eveline Shayo, akichangia hoja, katika kikao kilichojumuisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma.
Picha ni baadhi ya watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara - Mtumba, Novemba 11, 2026, Dodoma.
Maoni
Chapisha Maoni