BI. MEENA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI KOREA

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, Novemba 6, 2026 ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Korea uliopo katika Jiji la Seoul, ambako alikutana na kusalimiana na Balozi Noel Kaganda pamoja na baadhi ya watumishi wa ubalozi huo, ziara hiyo ambayo imelenga kufahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na ubalozi huo katika kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Korea.

Aidha, katika ziara hiyo, Bi. Meena alipokea nakala za Gazeti la Tanzanite, ambalo ni gazeti rasmi la Ubalozi wa Tanzania nchini Korea, linalosambaza taarifa kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania na Korea, zikiwemo fursa za biashara, uwekezaji na maendeleo.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI