BI. MEENA ATEMBELEA TAASISI YA KIOST KUKAGUA MAENDELEO YA MATUMIZI YA SATELAITI KATIKA BAHARI NA UVUVI
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, Novemba 2, 2026 ametembelea Taasisi ya KIOST iliyopo nchini Korea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Hyi-Seung Lee, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano katika matumizi ya teknolojia ya satelaiti kwenye sekta ya bahari na uvuvi.
Katika ziara hiyo, Bi. Meena ametembelea kituo cha kupokelea na kuchakata takwimu za satelaiti, ambapo amepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika kituo hicho, hususan matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji na uchakataji wa taarifa zinazohusiana na bahari na uvuvi.
Aidha, Bi. Meena ameshiriki katika mkutano wa kupokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Kuanzisha Kituo cha Matumizi ya Satelaiti kwenye Bahari na Uvuvi, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na KIOST, kwa lengo la kuimarisha matumizi ya teknolojia na takwimu za satelaiti katika maendeleo ya sekta ya bahari na uvuvi.




Maoni
Chapisha Maoni