BI. MEENA AFUNGUA MKUTANO WA KUTATHMINI MAENDELEO YA MRADI WA MATUMIZI YA SATELAITI KWENYE USIMAMIZI WA BAHARI NA UVUVI

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, Novemba 2, 2026 amefungua rasmi mkutano wa kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Matumizi ya Satelaiti katika Usimamizi wa Bahari na Uvuvi, unaolenga kuimarisha matumizi ya teknolojia ya satelaiti katika usimamizi wa rasilimali za bahari na sekta ya uvuvi nchini.

Mkutano huo umewakutanisha watekelezaji wa mradi kutoka Korea, wakiwemo Taasisi ya Sayansi ya Bahari na Teknolojia ya Korea (KIOST), Kampuni ya Underwater Science and Technology (UST21) na Kampuni ya Mirasea, inayoratibu miradi ya ODA ya uvuvi nchini Korea, pamoja na wataalamu kutoka Tanzania kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI