WAZIRI DKT. BASHIRU AZINDUA BENKI YA USHIRIKA TAWI LA KAGERA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amezindua Benki ya Ushirika (COOP BANK) tawi la Mkoa wa Kagera  na kufanya benki hiyo kufikisha matawi saba nchi nzima tangu kuanzishwa kwake, matawi mengine ni pamoja na Mtwara, Tandahimba, Dodoma, Dar es Salaam, Moshi na Tabora.

Uzinduzi wa benki hiyo umefanyika leo Agosti 18, 2026, katika Manispaa ya Bukoba, lilikiwa ni tawi la kwanza kufunguliwa kwa Kanda ya Ziwa na kubainisha kuwa uchumi wa sasa unahitaji jitihada za pamoja kupitia ushirika  kwa kwamba benki hiyo itaufufua ushirika kupitia sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa vyama vya ushirika kujikita zaidi katika sekta za uzalishaji hususan kuongeza thamani ya bidhaa na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, madini ili kuwa na tija ya kujikwamua kiuchumi, pamoja na kuondokan na umaskini huku akiwataka vijana na wanawake kuanzisha na kujiunga  na vyama vya ushirika katika sekta za mifugo na uvuvi.

"Katika dunia ya sasa ili mpige hatua ni lazima mshirikiane, kwa hiyo Coop Bank msaidie kuufufua ushirika ikiwemo katika mkoa huu wa Kagera ambao uchumi wake unategemea zaidi vyama vya ushirika, lakini pia nitoe rai kwa vijana na wanawake kujiunga na ushirika ili waweze kukopesheka na kupata mitaji. "

Vilevile, katika hotuba yake Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa rai  kwa Benki ya Ushirika (Coop Bank) kubuni miradi yenye tija na mikopo nafuu yenye masharti yanayoendana na uwezo wa wafugaji, wavuvi, wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

Kwa upande Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Yahya Ramadhani Kiddo, amesema mkoa huo una mazingira mzuri kwa ajili ya uwekezaji  na biashara na matarajio yao benki hiyo itawafikia wadau wengi zaidi katika sekta kilimo, mifugo na uvuvi.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Bw. Godfrey Ng'urah amesema kuwa katika kipindi cha robo ya mwaka 2026, benki hiyo imetoa zaidi ya shilingi bilioni 76 ikiwa ni sawa asilimi 60 kwa vyama vya ushirika kuongeza thamani, kupata zana za kilimo, pembejeo na masoko ya mazao baada ya mavuno ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 6 zilitolewa kwa sekta za mifugo na uvuvi, ambapo shilingi bilioni 5 zilitolewa kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwa vizimba na zaidi ya bilioni 2 kuongeza thamani ya maziwa na chakula huku lengo la benki hiyo ni kuwafikia watu milioni 10 na kuwahudumia kwa njia ya digitali ifikapo 2030.

Naye, Mwenyekiti wa Juhudi Amcos, Donald Emmanuel, amesema chama hicho kimenufaika na mikopo ya benki hiyo, ikiwemo shilingi bilioni 1.5 mwaka 2025 kwa ajili ya ukusanyaji wa kahawa na shilingi bilioni 5 mwaka 2026, ambapo asilimia 75 tayari imelipwa kwa wakulima.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa sita kutoka kulia) akikata utepe wakati wa kuzindua Benki ya Ushirika (COOP BANK) Tawi la Mkoa wa Kagera, hafla iliyofanyika Manispaa ya Bukoba, leo Agosti 18, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumzia umuhimu wa ushirika kiuchumi wakati wa uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tawi la Mkoa wa Kagera leo Agosti 18, 2026.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Kanali Yahaya Ramadhan Kido akieleza jinsi Mkoa huo ulivyotayari kwa uwekezaji na biashara wakati wa uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tawi la Mkoa wa Kagera leo Agosti 18, 2026.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika Bw. Godfrey Ng'urah akizungumzia juu ya hatua zinazofanywa na benki hiyo kuwa wezesha wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiariamali kupitia ushirika, wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Agosti 18, 2026.

Baadhi ya Wananchi na wanachama wa vyama vya ushirika wakiwemo wanachama wa Benki ya Ushirika (COOP BANK) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa benki hiyo iliyofanyika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Agosti 18, 2026.

Balozi wa Benki ya Ushirika Bw. Emanuel Mgaya maarufu kwa jina la ' Masanja Mkandamizaji akifurahia na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa baada kupata zawadi (kuokota) kutoka kwa waziri wakati wa uzinduzi wa Benki ya Ushirika leo Agosti 18, 2026 Mkoani Kagera.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD