Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amekutana na wawekezaji wa Kampuni ya XI
WANG GROUP kutoka nchini China kwa lengo la kujadiliana namna kampuni hiyo inaweza kufanya uwekezaji kwenye sekta ya
mifugo hususan uzalishaji wa vyakula vya mifugo hapa nchini.
Prof. Shemdoe amekutana na
wawekezaji hao mapema ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo Februari 7, 2024.
Wawekezaji hao
walioambatana na Mbunge wa Madaba, Dkt. Joseph Mhagama wametambulisha mradi wao
kwa Prof. Shemdoe ambao lengo lake ni kufanya uzalishaji wa mazao ya Soya,
Mahindi na Ufuta kwa ajili ya chakula cha mifugo katika shamba la mifugo la
Hanga Ngadinda lililopo Halmashauri ya Madaba, mkoani Ruvuma.
Pia, watawawezesha wakulima
wadogo kulima mazao hayo kwa wingi kwa ajili ya kutengenezea chakula cha
mifugo.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe aliwahakikishia ushirikiano wawekezaji hao ili sekta
ya mifugo iweze kuwa na mchango mkubwa katika pato la mtu mmoja mmoja na taifa
kwa ujumla.
Wawekezaji hao ni Bw. Si Ya
Feng na Bw. Yan Lei ambao wote ni Wakurugenzi kwenye kampuni hiyo ya XI WANG
GROUP.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiongea na Wawekezaji wa
Kampuni ya XI WANG GROUP alipokutana nao mapema ofisini kwake Mtumba, jijini
Dodoma leo Februari 7, 2024.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiongea na Wawekezaji wa
Kampuni ya XI WANG GROUP muda mfupi baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika
ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo Februari 7, 2024. Wa tatu kutoka
kushoto ni Mbunge wa Madaba, Dkt. Joseph Mhagama.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Wawekezaji wa Kampuni ya XI WANG GROUP muda mfupi baada ya kufanya nao
mazungumzo ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo Februari 7, 2024. Wa tatu
kutoka kushoto ni Mbunge wa Madaba, Dkt. Joseph Mhagama. Wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi, Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madalla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni