Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambaye ndio
Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi
linalojengwa katika mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma kuhakikisha
wanatumia malighafi zinazozalishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini.
Ulega ametoa maelekezo hayo
alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo Januari 7,
2024 ambapo aliambatana na timu ya Wataalamu wa Wizara.
“Nimekagua hapa nimeona
vipo vinavyozalishwa hapa nyumbani na nyinyi ni shirika la kizalendo lakini
ajabu sana mmeacha kununua vitu vya hapa nyumbani mmeamua kwenda kununua
vilevile ambavyo vinapatikana hapa nchini, na mkumbuke hamjengi nyumba ya mtu
binafsi ni ya umma”, alisema
Mhe. Ulega ametoa rai kwa
shirika hilo kama wanachofuata huko nje ni ubora au mtindo, wakutane na
wazalishaji waliopo hapa nchini na kuwaelekeza ubora na mitindo wanayoitaka ili
waweze kuzalishiwa.
Aidha, Waziri Ulega
amemtaka Mshauri Elekezi wa jengo hilo (TBA) kuhakikisha anamaliza ujenzi huo
Mei 31, 2024 kama mkataba unavyowataka.
Fundi Mkuu, kutoka Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia, Remigius Mwijage akimpa maelezo ya mchoro wa
jengo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alipofanya ziara ya
ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi
unaondelea katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo Januari 7, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Sera na
Mipango, kutoka Wizara ya Ardhi na Mendeleo ya Makazi, Bw. Amos Zephania (wa
pili kutoka kulia) na Mshauri Mwelekezi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Injinia, Weja Ng’olo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya
ujenzi wa jengo hilo leo Januari 7,2024. Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Daniel
Mushi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi,Mkandarasi pamoja na Mshauri Mwelekezi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya
Mifugo na Uvuvi alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo
hilo leo Januari 7,2024. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni