Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amekutana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi kujadiliana utekelezaji wa makubaliano ya kuendeleza mradi wa Afya Moja unaoangalia magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwenye Mifugo kwenda kwa binadamu ikiwepo Brucellosis na Kifua Kikuu (TB).
Prof. Shemdoe amekutana na
Mwakilishi huyo Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma Januari 7, 2024.
Mradi huo unasimamiwa na
Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Maprofesa kutoka Chuo cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) na Maprofesa kutoka Chuo cha Mifugo cha Rakuna, kilichopo
katika Mji wa Hokaido nchini Japan.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa
Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi (kulia) alipokutana nae
Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma Januari 7, 2024.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi
(kushoto) baada kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Mtumba,
jijini Dodoma Januari 7, 2024.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (katikati)akiagana na Mwakilishi Mkaazi
wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi (kushoto) muda mfupi
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Mtumba, jijini
Dodoma Januari 7, 2024.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni