Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. pius Mwambene akiongea na wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji bora wa ngombe wa maziwa chini ya mradi wa maziwa faida yaliyofanyika LITA Kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga, Septemba 29,2023
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Ushauri kutoka Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Bw. Joseph Msemwa akitoa utambulisho wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji bora ngombe wa maziwa , chini ya mradi wa maziwa faida uliofanyika LITA kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga, Septemba 29,2023
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Mashariki na Mratibu Mkuu wa Mradi wa Maziwa Faida Tanzania, Dkt. Zabron Nziku akieleza juu ya mradi huo kwa wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza walioudhuria mafunzo ya ufugaji bora wa ngombe wa maziwa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga. Septemba 29,2023
Afisa
Mahusiano wa Mradi wa Maziwa faida Dkt. Sizya Lugeye akiwasisitiza wafugaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kusikiliza kwa makini yale yote wanayofundishwa
na kuuliza maswali yanayowatatiza katika suala zima la ufugaji wa ng'ombe wa
Maziwa ili waweze kuboresha katika ufugaji wao wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya
Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Buhuri Mkoani Tanga Septemba 29, 2023
Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya (DALFO) Bw. Edward Mgaya akiwapongeza wafugaji kwa mwitikio mkubwa wa kushiriki mafunzo ya ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Buhiri Tanga , Septemba 29,2023
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo ya ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Muheza wakimsikiliza kwa
makini Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. Pius Mwambene
(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye
kampasi ya Buhuri mkoani Tanga Septemba 29,2023.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. Pius Mwambene (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na wafugaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Muheza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji bora wa ng'ombe wa
maziwa chini ya Mradi wa maziwa faida uliofanyika LITA Kampasi ya Buhuri Mkoani
Tanga, Septemba 29,2023
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni