Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (Kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo Dr.Olivia Kamana (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao cha ndani leo tarehe 13 Sept 2023 Jijini Kigali nchini Rwanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kutoka kushoto), leo tarehe 13 Sept 2023 akiambatana na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi walioshiriki Mkutano wa kuandaa andiko la Mradi wa kuongeza Uzalishaji wa Maziwa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza gesi joto kwa nchi za Africa mashariki,wamemtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo Dr.Olivia Kamana, Kigali nchini Rwanda (wa pili kutoka kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa na Wenyeji wao kutoka Rwanda, wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo Dr.Olivia Kamana (wa tatu kutoka kulia), Wengine katika picha ni wakurugenzi kutoka Rwanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe (kulia) wakijadiliana Mambo mbalimbali yahusuyo Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo wa Rwanda Dr.Olivia Kamana leo tarehe 13 Sept 2023 ofisini kwake jijini Kigali nchini Rwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni