Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2023

AFRICAN’S FOOD SYSTEMS FORUM 2023

Picha
 

DKT. SAMIA: UCHUMI WA BULUU NI FURSA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, uchumi wa buluu ni fursa huku akiwataka wananchi  kujipanga na kuweka mazingira muafaka ya  uwekezaji ili waweze kunufaika kupitia rasilimali zinazopatikana katika sekta hiyo. Dkt. Samia alisema hayo katika  sherehe za Msimu wa Pili wa Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Sea Food Festival) lililofanyika katika ufukwe wa Kendwa, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar Juni 23, 2023. Wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Rais, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  alisema maana halisi ya uchumi wa buluu ni matumizi endelevu ya rasilimali zilizomo kwenye bahari, maziwa na mito kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa, kutengeneza ajira na kuleta ustawi wa maisha ya watu na vilevile kutunza afya ya maumbile ya bahari. Alisema kupitia tamasha hilo ni muhimu kujizatiti na kujipanga vyema ili kuweza kuzitumia fursa zilizopo na zinazojitokeza katika sekta ya uchumi wa buluu. Aliongeza kwa kusema kuwa ...

SERIKALI YA DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Picha
Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini. Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023. Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu. "Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema  Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu. Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kuj...

UTALII WA BAHARI KUNUFAISHA WAVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema  Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira mazuri kupitia fursa za Utalii wa Bahari ili wavuvi hasa  wadogo waweze kunufaika kwa kuuza samaki na mazao yake. Waziri Ulega alisema hayo wakati wa tukio la mashindano ya Ngalawa (Ngalawa race) lililofanyika kwenye ufukwe wa Kendwa uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja Juni 22, 2023. Alisema kuwa kupitia mashindano hayo shughuli za uvuvi zitatangazika duniani na kuvuta watalii wengi na  hivyo wavuvi  watapata fursa nzuri ya  kufanya biashara ya samaki. Aliongeza kuwa mashindano hayo yanachagiza ujio wa watalii nchini na hivyo kupelekea utalii wa bahari  kushamiri kitendo ambacho kinaongeza fursa ya biashara kwa  wavuvi. "Tunataka huu utalii wa bahari  uwanufaishe moja kwa moja wavuvi wadogo waweze kupata kipato chao kutokana na mauzo ya samaki na mazao yake kwa watalii hao," alisema Aidha, Mhe. Ulega aliwashauri w...

SERIKALI YA RAIS, DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Picha
Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini. Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023. Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu. "Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema  Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu. Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ...

SERIKALI YA DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Picha
Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini. Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023. Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu. "Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema  Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu. Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kuj...

​SERIKALI YAENDELEA KUTEKELEZA MPANGO WA UFUGAJI WA KISASA NA KIBIASHARA – SILINDE

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. David Silinde amesema serikali inaendelea kutekeleza mpango wa kuhakikisha wafugaji wanafuga kisasa na kibiashara ili kuongeza tija kwa wafugaji na mchango wa Sekta ya Mifugo kwenye pato la taifa.   Silinde ameyasema hayo leo (17.06.2023) wakati akifungua mafunzo yenye Kauli Mbiu ya “Youth Bussiness Engangement Through Livestock” kwa vijana wajasiriamali wanaonenepesha mifugo kupitia vituo atamizi, Kampasi ya LITA Kikulula, Karagwe.   Katika kufanikisha utekelezaji wa mpango huo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliandaa mwongozo ambao umeainisha majukumu ya wadau mbalimbali walioko katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mifugo. Kwa upande wa taasisi za fedha ikiwemo mabenki, Wizara, pamoja na mambo mengine, inawategemea kusaidia kubadilisha fikra na mitazamo ya vijana kuwa ya kibiashara ili kuweza kutengeneza fursa nyingi zaidi za ajira kupitia sekta ya mifugo; pamoja na kuwafundisha namna ya kuandaa ...

WANUFAIKA WA MIKOPO YA UFUGAJI SAMAKI WAPATIWA MAFUNZO

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amewataka wanufaika wa mikopo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kuhakikisha wanazingatia mafunzo ya utekelezaji wa miradi hiyo kitaalam ili iweze kuwaletea maendeleo na kuweza  kurejesha mikopo kwa wakati Mhe. Sima alisema hayo Juni 14 mwaka huu wakati akifungua mafunzo kwa vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi wanaotarajiwa kunufaika na mkopo wa masharti nafuu usio na riba ukijumuisha pembejeo za vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki Mkoani Kagera Aliseme lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa mikopo hiyo ni kutatua changamoto iliyopo kwa wananchi husasani ukosefu wa mitaji na upungufu wa samaki ziwani. "Hakikisheni mnazingatia utaalamu katika usimamizi, mbegu bora ya samaki mtakaopandikiza, ulishaji wa samaki kwa kutumia chakula bora, ulinzi wa vizimba na biashara kwa kuzingatia taarifa za soko" alisema Mhe. Sima Aidha alibainisha kuwa Serikali imeshatenga maeneo ya...

FETA YATAKIWA KUTANUA WIGO WA MASHIRIKIANO KATIKA KUTOA MAFUNZO

Picha
Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) imetakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano katika kutoe elimu ya uvuvi.   Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh wakati akifunga mafunzo ya siku 30 ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchini Somali, mafunzo ambayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.   Prof. Sheikh amesema kuwa FETA inatakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano na nchi mbalimbali kwani zipo rasilimali nyingi na wataalam wapo wa kutosha hivyo haitakiwi wataalam kujifungia wenyewe badala yake wajitokeze na kuhakikisha wanatoa mafunzo ili kuongeza utaalam kwenye utekelezaji wa shughuli za uvuvi.   Vilevile amewasihi kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo kwa watu wa ndani na nje ya nchi hasa wanaijishughulisha na shughuli za ...

NYAMA YA TANZANIA KUANZA KUUZWA MISRI

Picha
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na ujumbe kutoka Misri wakati wa kikao kifupi cha asubuhi "Breakfast Meeting" kilichofanyika jijini Dodoma mapema leo Juni 12, 2023. Ujumbe kutoka nchini Misri uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Huduma za Miradi (NSPO) Meja Jenerali, Hossam Nigeda ( kushoto kwa Mhe. Waziri). Waziri Ulega alikutana na ujumbe  huo kujadiliana namna ya kuanza kufungua soko la nyama ya Tanzania nchini Misri. Katika mazungumzo yao, Meja Generali, Nigeda alimueleza Mhe. Ulega kuwa lengo lao ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili kwa kufungua soko la nyama ya Tanzania nchini Misri. Aliongeza kuwa wamejipanga kuanzisha machinjio ya kisasa hapa nchini ambayo itawawezesha kusafirisha Tani Mia Sita (600) ya nyama kila Mwezi, pia kusafirisha wanyama hai wakiwemo ng'ombe, Kondoo na Mbuzi Elfu Kumi (10,000) kila Mwezi. Alifafanua kuwa kwa siku za hivi karibuni wapo katika mipango ya kusafirisha Tani ...

ELIMU YA UANDAAJI NA UHAULISHAJI WA SAMAKI WANAOFUGWA KWENYE VIZIMBA YATOLEWA

Picha
  Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Frederick Mussa akitoa elimu ya  uhandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika (hawapo pichani) wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa,Wilaya ya Sengerema Mkoani  Mwanza, Juni 08,2023. Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya dawati la Sekta binafsi, Mwalimu Ambakisye Simtoe akitoa elimu juu ya ujasiliamali, marejesho ya mikopo na utunzaji wa kumbukumbu  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa, Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, Juni 08,2023 Afisa Uvuvi  Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi  (kushoto) akiwaelekeza kwa  vitendo jinsi ya kutengeneza kizimba wanufaika wa mkopo...

JUHUDI ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KULINDA BAHARI- DKT. MPANGO

Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema zinahitajika juhudi za pamoja za ndani ya nchi, kikanda na kimataifa katika kuweka mikakati ya kulinda rasilimali za bahari vinginevyo ifikapo mwaka 2050 bahari itakuwa imeelemewa.    Makamu wa Rais alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 08 Juni 2023.  Alisema inapaswa kuwepo kwa uwiano sawia kati ya hali ya bahari na kuimarika kwa uchumi kwani Afya ya Bahari na mifumo imara ya kiikolojia ya baharini ni muhimu kwa uchumi wa buluu ambao ni sehemu ya ajenda ya nchi kufikia maendeleo endelevu. Dkt. Mpango aliongeza kwamba tafiti zinaonesha kufikia 2030 Bahari itakuwa ndio nguzo kuu ya uchumi duniani ambapo takriban watu milioni 40 watakuwa wameajiriwa moja kwa moja na viwanda vinavyotumia rasilimali za bahari.   Aidha, Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Wizara ya Mifugo na Uvuvi...
Picha
 SHEKHE WALID, MCHUNGAJI MWAMPOSA MABALOZI UHIFADHI WA BAHARI  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema Wizara yake itawatumia Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Walid Alhad Omar na Mchungaji wa Kanisa la Arise and Shine na Boniface Mwamposa kuwa mabalozi wa uhifadhi wa Bahari ili wasaidiane nao katika kuelimisha jamii hasa zinazoishi kando ya Bahari juu ya athari ya uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira ya Bahari kwa ujumla. Waziri Ulega alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 8, 2023. Alifafanua kuwa pamoja na uwepo wa Sheria  kwenye usimamizi na uendelevu wa rasilimali za Bahari, ni muhimu pia kushirikiana na jamii katika kuhakikisha mazingira ya Bahari yanahifadhiwa vizuri kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha jamii wameamua kuwatumia Viongozi hao wa Dini kuwa mabalozi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuepuka vitendo ambavy...

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANUFAIKA WA MIKOPO YA VIZIMBA YAENDELEA NCHINI

Picha
  Mteknolojia wa samaki mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Hamidu Njengite akitoa elimu kuhusu mikopo isiyo na riba ya pembejeo za zao la Mwani kwa wakulima wa zao hilo waliopo kata ya Mchinga mkoani Lindi Juni 08, 2023 Sehemu ya wakulima wa zao la Mwani kutoka kata ya Mchinga mkoani Lindi wakisoma mwongozo wa kilimo cha zao hilo waliopewa na timu ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  iliyofika hapo Juni 08, 2023 kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao la Mwani. Katibu  Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Bw. Emil Kasagara akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa hao kufika ofisini kwake, kumuelezea juu ya ujio wao wa kuwajengea uwezo wanufaika wa mkopo wa vizimba wenye masharti nafuu na usio na riba katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mkoani Mwanza, Juni 07,2023 Picha ya pamoja ya wanavikundi wa "Busumi fishing corporation So...