Nav bar

Jumapili, 11 Juni 2023

ELIMU YA UANDAAJI NA UHAULISHAJI WA SAMAKI WANAOFUGWA KWENYE VIZIMBA YATOLEWA

 

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Frederick Mussa akitoa elimu ya  uhandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika (hawapo pichani) wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa,Wilaya ya Sengerema Mkoani  Mwanza, Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya dawati la Sekta binafsi, Mwalimu Ambakisye Simtoe akitoa elimu juu ya ujasiliamali, marejesho ya mikopo na utunzaji wa kumbukumbu  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Buchosa, Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, Juni 08,2023


Afisa Uvuvi  Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi  (kushoto) akiwaelekeza kwa  vitendo jinsi ya kutengeneza kizimba wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza  Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mkomanile Mahundi akitoa elimu juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu ufugaji wa samaki kwa vizimba  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye Halmashauri ya Buchosa, Wilaya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 08, 2023.


Timu ya watoa mafunzo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Buchosa, Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 08,2023


Mkurugenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Bunda, Eng. Emmanuel Mkongo (aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Afisa uvuvi wa Mkoa wa Mara, walipoenda kutembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha walipoenda kutoa mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa wanufaika wa mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), June 08.2023.


Afisa Uvuvi wa Mji wa Bunda, Bw. Reginald shirima, akiongea na wanufaika wa mikopo ya riba nafuu ya vizimba na pembejeo za ufugaji samaki kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba, katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoani Mara, Juni 08,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Janeth Rukanda akizungumza kwa nyakati tofauti na baadhi wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya za Muheza na Pangani Mkoani Tanga ambao wamefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo amesema wanavikundi hao wameonesha utayari wa kupokea mikopo hiyo na kulima zao la mwani kwa tija. (08.06.2023)


Afisa Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji Tanga Bw. Onesmo Mwanyumba (fulana nyeupe) akiwaelekeza baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Muheza na Pangani Mkoani Tanga ambao wamefanikiwa kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), namna ya ufungaji bora wa zao hilo ili lisiharibike au kupotea likiwa baharini (08.06.2023)


Baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wakijifunza njia bora ya kufunga zao la mwani ili lisikatike na kupotea likiwa baharini baada ya kupatiwa mafunzo na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuatia baadhi ya vikundi hivyo kukubaliwa ombi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambapo wanavikundi 200 wamenufaika na mafunzo hayo katika Mkoa wa Tanga. (08.06.2023)


Afisa Uvuvi Kata ya Pangani Mashariki katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Bw. Salim Said Mohamed, akifafanua kwa baadhi ya wanavikundi wanaojishughulisha na kilimo cha mwani, namna serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilivyoamua kuwekeza kwenye vikundi hivyo ili kuhakikisha zao la mwani linalimwa kwa wingi na kuongeza pato kwa nchi na mwananchi mmoja mmoja kufuatia kukubaliwa kwa ombi la baadhi ya vikundi la kupatiwa mkopo usio na riba kutoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (08.06.2023)


Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa mafunzo ya Ujasiliamali, Usimamizi wa Biashara na mikopo kwa vyama vya Ushirika ,vikundi,makampuni na watu binafsi  wanaojihusisha na Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza ambao wanatarajia kupata mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambapo watapatiwa vizimba na pembejeo za ufugaji samaki. mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Fadhili Ruzika,akitoa elimu ya  uandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika  wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye ukumbi wa Halmashauri Wilaya ya Ukerewe Mkoani  Mwanza, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Titus Kilo, akiongea na wanufaika wa mikopo ya riba nafuu ya vizimba na pembejeo za ufugaji samaki kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba, katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya Wilayaya Ukerewe, Mkoani Mwanza, Juni 09,2023.


Sehemu ya wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba unaotarajiwa kutolewa na Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki  wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa uvuvi (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Ufugaji Samaki kwa njia ya vizimba kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Ukerewe Mkoani Mwanza, Juni 09,2023.


Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Happy Kapinga akiwapa elimu wakulima wa zao la mwani waliopo Kilwa Masoko mkoani Lindi kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao hilo Juni 09, 2023.


Sehemu ya wakulima wa zao la Mwani waliopo Wilaya ya Kilwa Masoko mkoani Lindi wakisikiliza maelekezo ya mtaalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hayupo) kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao hilo Juni 09, 2023.


Katibu Tawala Mkoa wa Geita Prof. Godius Kanyarara akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) na Mkoa wa Geita mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika ofisini kwake,  lengo likiwa ni pamoja na kueleza nia ya Wizara hiyo kwa kushirikiana  na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) ya kutoa mkopo wenye masharti  nafuu isiyo na riba kwa vikundi, vyama vya ushirika na watu binafsi ikijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki, Mkoani Geita, Juni 09,2023


Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Geita - Nzera, Mkoani Geita, Juni 09,2023


Timu ya Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakikagua nyavu ambayo itatumika kutengenezea kizimba, wakati walipoenda kuangalia maendeleo ya utengenezaji wa vizimba kwa mmoja wa wazabuni walioshinda tenda ya kusambaza vizimba hivyo kwa wanufaika wa mikopo nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), katika Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, Juni 10,2023.


Muonekano wa Nyavu ambazo ziko tayari kufungwa kwenye fremu za Vizimba vitakavyosambazwa , kwa  wanufaika wa mikopo nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ambazo zinaendelea kutengenezwa kwa mzabuni kampuni ya KCG AQUATEC aliyeshinda tenda ya kusambaza vizimba hivyo, iliyopo Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu, Juni 10,2023.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni