Nav bar

Jumanne, 27 Juni 2023

SERIKALI YA RAIS, DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Katika hatua za kutekeleza mikakati  ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini.


Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023.


Wakati  wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji  wa Sera ya Uchumi wa Buluu.


"Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema 


Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu.


Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kujiokolea Mia moja (100), Gps Nne (4) ambapo vifaa hivyo vitatumiwa na vyombo 25.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni