Nav bar

Jumapili, 11 Juni 2023

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANUFAIKA WA MIKOPO YA VIZIMBA YAENDELEA NCHINI

 

Mteknolojia wa samaki mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Hamidu Njengite akitoa elimu kuhusu mikopo isiyo na riba ya pembejeo za zao la Mwani kwa wakulima wa zao hilo waliopo kata ya Mchinga mkoani Lindi Juni 08, 2023

Sehemu ya wakulima wa zao la Mwani kutoka kata ya Mchinga mkoani Lindi wakisoma mwongozo wa kilimo cha zao hilo waliopewa na timu ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  iliyofika hapo Juni 08, 2023 kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu mkopo usio na riba wa pembejeo za zao la Mwani.

Katibu  Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Bw. Emil Kasagara akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa hao kufika ofisini kwake, kumuelezea juu ya ujio wao wa kuwajengea uwezo wanufaika wa mkopo wa vizimba wenye masharti nafuu na usio na riba katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Picha ya pamoja ya wanavikundi wa "Busumi fishing corporation Society" na Bwai Fisheries, vinavyojishughulisha na Uvuvi katika Halmashauriya ya Musoma Vijijini (DC), wakiwa na maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkoa wa Mara, baada ya kupatiwa mafunzo mafupi juu ya Ufugaji wa Vizimba  na namna bora ya kuimarisha vikundi vyao wakati wakisubiri kukamilika kwa taratibu za kupatiwa mkopo usio na riba ambao waliomba kutoka serikalini na kukubaliwa ombi lao. Mkopo utatolewa kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). (07.06.2023)

Afisa Uvuvi mwandamizi Bw. Clemence Katunzi (kulia) akitoa elimu  juu ya mfumo wa M-Kilimo kwa baadhi ya maafisa Uvuvi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023


Sehemu ya wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba unaotarajiwa kutolewa na Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki  wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa uvuvi (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika  kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi  Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Clemence Katunzi  akiwaelekeza kwa  vitendo jinsi ya kutengeneza kizimba wanufaika wa mkopo  wenye masharti  nafuu usio na riba kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi (Uvuvi) kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ukijumuisha  Pembejeo za  vizimba, chakula cha samaki na vifaranga vya samaki   kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya dawati la Sekta binafsi, Mwalimu Ambakisye Simtoe akitoa elimu juu ya ujasiliamali, marejesho ya mikopo na utunzaji wa kumbukumbu  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani wa Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bw. Fredrick Mussa akitoa elimu ya  uhandaaji na ulishaji wa samaki wanaofugwa kwenye vizimba  wakati wa  mafunzo ya Ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi kwenye  Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani wa Mwanza, Juni 07,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mkomanile Mahundi akitoa elimu juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu ufugaji wa samaki kwa vizimba  kwa wanufaika wa mkopo wa vizimba na pembejeo zake kwa vyama vya Ushirika, Vikundi na watu binafsi (hawapo pichani) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Juni 07,2023

Maafisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Afisa uvuvi Mkoa wa Mara wakiwa kwenye ofisi ya kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Musoma vijijini,Bw. Magange Mwita (wapili kushoto) ikiwa lengo ni kujitambulisha na kutoa dhumuni la kufika kutoa mafunzo katika Wilaya hiyo kwa wanufaika wa mikopo ya vizimba na pembejeo zake, ambapo mikopo hiyo imetoka serikalini kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). tarehe (07.06.2023)

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Dawati la Sekta binafsi chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Eliakim Mniko  akitoa mafunzo ya Ujasiliamali, Usimamizi wa Biashara na mikopo kwa vyama vya Ushirika ,vikundi,makampuni na watu binafsi (hawapo pichani) wanaojihusisha na Uvuvi katika Halmashauri ya Wiala ya Musoma Vijijini,  Mkoa wa Mara ambao wanatarajia kupata mikopo ya riba nafuu kutoka serikalini kupitia benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambapo watapatiwa vizimba na pembejeo za ufugaji samaki.(07.06.2023)


Wanufaika wa mikopo ya vizimba na pembejeo zake kutoka Halmashauri ya Wilaya Musoma Vijijini wakiuliza maswali kuhusu upatikanaji wa mikopo iliyotolewa na serikali, kwenye mafunzo ya Ufugaji Samaki kwenye vizimba kutoka kwa maafisa uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani). (07.06.2023).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni