Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) imetakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano katika kutoe elimu ya uvuvi.
Hayo
yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed
Sheikh wakati akifunga mafunzo ya siku 30 ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao
ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchini Somali,
mafunzo ambayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi
Kampasi ya Mbegani wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Prof.
Sheikh amesema kuwa FETA inatakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano na nchi
mbalimbali kwani zipo rasilimali nyingi na wataalam wapo wa kutosha hivyo
haitakiwi wataalam kujifungia wenyewe badala yake wajitokeze na kuhakikisha
wanatoa mafunzo ili kuongeza utaalam kwenye utekelezaji wa shughuli za uvuvi.
Vilevile
amewasihi kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kuendesha
mafunzo hayo kwa watu wa ndani na nje ya nchi hasa wanaijishughulisha na
shughuli za uvuvi.
Wataalam
wa uvuvi kutoka Somalia wamekuwa wakishiriki mafunzo hayo hapa nchini kwa lengo
la kuongeza uwezo katika kusimamia rasilimali za uvuvi na kuhakikisha kuwa kuna
kuwa na uvuvi endelevu nchini kwao.
Prof.
Sheikh amesema upo umuhimu mkubwa katika kuhakikisha mazao ya bahari yanakuwa na
ubora unaotakiwa, hivyo ameitaka FETA kuhakikisha inaendela kuhamasisha na
kutoa mafunzo hayo kwa washiriki kutoka nchi mbalimbali.
Vilevile
amelishukuru Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwa kuwezesha kufanyika
kwa mafunzo hayo ambapo ameyaomba na mashirika mengine kuiga mfano huo ili
kuwezesha mafunzo hayo kuwafikia washiriki wengi zaidi.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dkt. Semvua
Mzighani amesema kuwa mafunzo yanayotolewa chuoni hapo msisitizo mkubwa huwa ni
kwenye kufanya mafunzo kwa vitendo hivyo ni matarajio yake kuwa watakaporejea
nchini kwao watakwenda kutekeleza yale waliyofundishwa kwa vitendo kitu ambacho
kitawaongezea ujuzi zaidi na kusaidia kutoa elimu kwa wengine.
Vyuo
vya vyao vinatoa mafunzo ya uhandisi katika maji, ubora wa samaki, uvuvi na
ubaharia, ukuzaji viumbe maji, mazingira na rasilimali za bahari, sayansi ya
bahari na menejimenti ya bahari.
Akiongea
kwa niaba ya wanafunzi wengine Rais wa wanafunzi hao kutoka chuo cha Uvuvi
nchini Somalia bwana Elm A. Mohamed alisema kuwa nchi zetu vyema zikashirikiana
katika rasilimali zetu kwani zinafanana hasa ukanda wa bahari pamoja na ufugaji
vilevile tushirikiane kati Nyanja za utamaduni kwani utamaduni wa watanzania ni
mzuri sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni