Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akitoa neno wakati wa kikao cha maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF) kilichofanyika Machi 16, 2023. Tukio hilo la uzinduzi litafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2023 na Mgeni rasmi atakuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika(AGRF), Bw. Amath Pathe Sene wakati wa kikao cha maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika(AGRF) kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akiwa katika meza moja na Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kikao cha maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika(AGRF) kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023.
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akimueleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kikao cha maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni