Nav bar

Jumamosi, 1 Aprili 2023

MAFUNZO KWA VITENDO (ATAMIZI) UVUVI KATIKA KITUO CHA MPANJU FISH FARM

 

Meneja wa kituo cha Mpanju Fish Farm Bw. Elpidius Mpanju akitoa maelezo kwa wataalamu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya namna wanavyofanya shughuli zao pamoja na vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo (Atamizi)(Hawapo pichani) waliowapokea kituoni hapo kilichopo Jijini Mwanza, Machi 16,2023.

Wataalam wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu wakizungumza na vijana wanaopata mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa vitendo kwenye kituo cha Mpanju Fish Farm kilichopo  Mwanza, lengo kujua wanaendeleaje na programu ya mafunzo hayo katika kituo hicho, Machi16,2023.

Picha ya pamoja ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu na vijana wanaopata mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa vitendo kwenye kituo cha Mpanju Fish Farm kilichopo  Mwanza  mara baada ya kukagua na kunzungumza na vijana hao. Machi16,2023)

Wataalam wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  wakiongea na vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo wa kituo cha Dkt.Charles Tizeba kilichopo Mkoani Mwanza,  Machi, 16.2023.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni