Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Emmanuel Bulayi akiongea wakati wa kikao na wawakilishi wa kampuni inayojihusisha na biashara ya taa za sola (WASSHA) pamoja na watendaji kutoka Sekta ya uvuvi (hawapo pichani) kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma Disemba 15,2022 lengo likiwa ni pamoja na kujadili namna ya kuzuiya teknolojia zisizofaa, kutoa elimu kwa wavuvi na kuzuiya Uvuvi haramu.
Mtendaji Mkuu wa kampuni inayojihusisha na biashara ya taa za sola (WASSHA), Bw. Satoshi Akita (katikati) akieleza juu ya taa hizo, bei na namna zinavyofanya kazi kwa watendaji wa Sekta ya uvuvi (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma Disemba 15,2022.
Sehemu ya washiriki wa kikao wakifuatilia kwa makini wasilisho lililokuwa likitolewa na Afisa Mkuu Mwendeshaji wa kampuni ya Kijapani inayojihusisha na biashara ya taa za sola (WASSHA), Bw. Tatsuki Yoneda (wa kwanza kushoto) kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma Disemba 15,2022.
Mkurugenzi wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bw. Emmanuel Bulayi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya Sola ya Japan (WASSHA) na watendaji kutoka Sekta ya Uvuvi mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa NBC Jijini Dodoma, Disemba 15,2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni