Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akimsikiliza mmiliki wa shamba la ndoto Bw. Hartmut Rottinger wakati alipomtembelea shamba kwake Mkoani Iringa Novemba 10,2022 lengo likiwa ni pamoja na kujifunza namna shughuli za ulimaji malisho na utunzaji wa Mifugo unavyofanyika.
Mmiliki wa shamba la Miombo Bw. Rex Fey akieleza namna anavyofanya kazi katika shamba hilo na aina ya malisho anayozalisha kwa Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda (katikati) wakati wa ziara yake katika shamba hilo lengo likiwa ni pamoja na kujifunza namna shughuli za uzalishaji wa malisho na Mifugo unavyofanyika shambani hapo, Novemba 10,2022 Mafinga Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda akiongea na watendaji wa shamba la Mifugo la SAOHILL wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi za shamba hilo lililopo Mafinga Mkoani Iringa Novemba 10,2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti, mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi uzalishaji wa Mifugo Bw. Simon Lyimo (kulia) pamoja na watendaji wa shamba la Mifugo la SAOHILL mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika shambani hapo Novemba 10,2022 Mafinga Mkoani Iringa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni