Mwakilishi wa Chemba ya Biashara kutoka Marekani Bw. Laurent Bou Anich (kulia) akimfafanulia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki kuhusu fursa za uwekezaji wanazotaka kufahamu kwa upande wa Sekta za Mifugo na Uvuvi nchini muda mfupi baada ya Ujumbe kutoka chemba hiyo na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kufika kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la NBC leo (11.11.2022).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( Tantrade) Bi. Latifa Khamis (kushoto) akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki miongoni mwa majarida ya fursa za uwekezaji yaliyoandalia na Chemba ya Biashara ya Marekani muda mfupi baada ya Bi. Khamis na ujumbe kutoka chemba hiyo kufika kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la NBC leo (11.11.2022)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (mbele) akifafanua fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta za Mifugo na Uvuvi mbele ya ujumbe kutoka Chemba ya Biashara ya Marekani na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( Tantrade) muda mfupi baada ya ujumbe huo kufika kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la NBC leo (11.11.2022) lengo la ziara hiyo likiwa ni kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni