Nav bar

Ijumaa, 28 Oktoba 2022

MAUZO YA NYAMA NJE YA NCHI YAONGEZEKA - DKT. MUSHI

Mauzo ya nyama nje ya nchi yameongezeka kutoka tani 1,774.00 mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani 10,415 katika mwaka 2020/2022.

Hayo yamesemwa na Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Dkt. Daniel Mushi Oktoba 28,2022 Jijini Dodoma wakati akieleza  utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema mwaka 2018/2019, waliuza tani za nyama 1,759 wakati mwaka 2019/2020 waliuza tani za nyama 692.46.

 “Kwa mwaka wa fedha uliopita tuliuza nyama nje ya nchi tani 10,415 ni kiasi ambacho hatujawahi kufikia kukiuza na hii imetupatia Sh96 bilioni...Kiasi kikubwa cha fedha kimepatikana kutokana na kuuza nyama nje ya nchi,”amesema.

Amesema katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 wameuza tani 3,256.60 za nyama nje ya nchi.

Amesema mkakati wao kwa mwaka 2022/2023 ni kuongeza kiasi cha nyama kinachouzwa nje ya nchi ambapo hadi sasa wanauza kwa kiasi kikubwa katika nchi za Mashariki ya Kati.

Amezitaja nchi zinazouzwa nyama kutoka Tanzania ni Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain, Kuwait, Oman, Comoro, Hong Kong, Jordan na Saudi Arabia.

Dkt. Mushi amesema lengo la bodi hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaongeza uuzaji wa nyama nje ya nchi hadi kufikia tani 16,000 kila mwaka ifikapo mwaka 2026.

Amesema kuwa takwimu zinaonyesha bado mtanzania mmoja anakula kilo 15 za nyama kwa mwaka badala ya kilo 50 zinazoshauriwa kitaalam.

“Watanzania wengi tunahitaji kuboresha afya zetu kwa kula nyama, kiasi ambacho kinachoruhusiwa na kupendekezwa,”amesema.

Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania (TMB), Dkt. Daniel Mushi  akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  Oktoba 28,2022 alipokutana nao kuzungumzia lengo na majukumu ya Bodi ya nyama  Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo (Dodoma).

SAUTI YETU WIKI HII

DKT. BITANYI AZUNGUNZIA MAJUKUMU YA WAKALA YA MAABARA YA VETERINARI TANZANIA

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo (Dodoma).

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari - Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi kuzungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo (Dodoma).

Meneja wa Wakala ya Veterinari Tanzania (TVLA) kituo cha Dodoma Dkt. Japhet Nkangaga (kushoto) akifuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Stella Bitanyi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari - Maelezo (Dodoma) kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari - Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UNITED GREEN KUTOKA UINGEREZA AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA - SEKTA YA MIFUGO

Mkurugenzi wa kampuni ya United Green, Bw. Rod Bassett kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania akiwasilisha mapendekezo kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022. kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma pamoja na binafsi za Tanzania.

Menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa Mifugo  na wataalamu kutoka Idara ya Biashara za kimataifa kutoka ubalozi wa uingereza nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao, kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma na binafsi za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye kikao cha menejimenti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi na wataalamu kutoka Ubalozi wa uingereza nchini Tanzania, (kushoto)  ni Mkurugenzi wa Kampuni ya United Green na (kulia) Mshauri wa biashara Bw. Godfrey Lwakatare, kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Serikali Mtumba, Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.

Sehemu ya menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo wakifatilia kwa makini mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na muwasilishaji (hayupo pichani) kwenye kikao kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya Mifugo na taasisi za Umma za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba,Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.

SAUTI YETU WIKI HII

Picha ya Pamoja ya Timu ya Wataalam toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiongozwa na Wakurugenzi wasaidizi  wa Ukuzaji Viumbe Maji Bahari  Dkt. Hamisi Nikuli watatu toka (kuli ), wa pili ni Mkurugenzi Masidizi wa Ugani wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Bw.Antony Dadu wa  pili toka (kulia), Bw.Augustine Mshanga Mchumi, wa kwanza (kulia) toka Dawati la Sekta Binafsi,Mtaalam wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ( TADB ) Bw.Richard Sempindu wa pili   toka ( kushoto ) na  katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni Bw.James Mkumbo picha imechukuliwa ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, lengo la ziara ya wataalam katika ofisi hiyo ni kujitambulisha kuwa wamekuja kwa kazi ya kuhakiki fomu za mikopo ya wadau wa uvuvi wanao kopeshwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Boti, na Vizimba (20.10.2022).

MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI

Jumatano, 26 Oktoba 2022

ULEGA: SOKO LA NYAMA LAFUNGUKA

 Serikali imesema kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuifungua  Nchi yetu, soko la nyama  limeongezeka kwa asilimia kubwa.

Akizungumza Oktoba 25, 2022 wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye Wilaya ya mbarali Mkoani  Mbeya, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb),  alisema mwaka 2021  Tanzania iliuza takribani tani 2000 tu za nyama  huku hadi kufikia sasa tayari tani 10000 za nyama zimeuzwa.

Alisema, kwa sasa soko la nyama nchini limeongezeka mara dufu nje ya nchi na kuwataka wafugaji kufuga kisasa   ili kukidhi hitaji la soko.

"Kwa mara ya kwanza Tanzania imeuza nyama nyingi nje ya mipaka, Mwaka  2021 mwezi Oktoba ni tani 2000 tu ndio  ziliuzwa, lakini mwaka huu Oktoba tayari tumeshauza tani zaidi ya 10000, hii ni kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu kutangaza kuwa tuna mifugo mingi na mizuri,

Bado fursa ya soko nje ya nchi ni kubwa, hivyo Wizara kwa kushirikiana na Serikali imeshatenga fedha za mashine kwa ajili ya kuchimba mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo, "alisema Mhe. Ulenga.

Aidha Mhe. Ulega aliwataka wafugaji kuunga mkono jitihada za Serikali ili kwa kushirikiana waweze kufuga kisasa, kwa tija na  kufikia malengo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na kamati ya mawaziri wa kisekta  wa kutatua migogoro ya ardhi wakati wa ziara yao  kwenye kata ya Ubaruku, tarafa ya Rujewa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Oktoba 25,2022.

Jumapili, 23 Oktoba 2022

ULEGA AKABIDHI MPANGO WA MABADILIKO WA SEKTA YA MIFUGO

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amemkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma Mpango wa Mabadiliko wa Sekta ya Mifugo.

Naibu Waziri Ulega amekabidhi mpango huo leo (19.10.2022) kwenye Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma ambapo Taarifa ya Tasnia ya Ngozi iliwasilishwa.

Akizungumzia kuhusu mpango huo, Naibu Waziri Ulega amesema kuwa Sekta ya Mifugo imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ambayo yatakwenda kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji kwa sasa zikiwemo za upatikanaji wa malisho, maji, majosho pamoja na afya ya mifugo kwa ujumla.

Pia amesema kuwa kwa Tanzania takribani kaya milioni nne hadi tano zinajishughulisha na shughuli za ufugaji hivyo kwa kutekeleza mpango huo kutawezesha kaya nyingi kuongeza kipato na kuwezesha ongezeko la mchango wa Sekta ya Mifugo kwenye Pato la Taifa.

“Sekta ya Mifugo ni Mgodi ambao ukiwekeza leo faida yake inarudi kwa haraka kwa kuwa Kaya takribani milioni nne hadi tano zinajihusisha na ufugaji wa kuku, ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na mifugo mingine hivyo kwa mpango huu tunatarajia utakwenda kufanikisha utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia wa kuwa na wafugaji badala ya wachungaji wa mifugo,” Alisema

“Lakini kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mpango huu tutahakikisha wadau wanashirikishwa ili waweze kutoa maoni yao yatakayosaidia kuuboresha zaidi,” aliongeza

Aidha, Wizara hiyo iliwasilisha taarifa ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) na Taarifa ya Tasnia ya Ngozi kwenye kikao hiyo ambapo wajumbe wa kamati waliweza kutoa michango yao ambayo Naibu Waziri Ulega aliwaahidi wajumbe kuwa Wizara itakwenda kuifanyia kazi.

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UNITED GREEN

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye kikao cha menejimenti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi na wataalamu kutoka Ubalozi wa uingereza nchini Tanzania, (kushoto)  ni Mkurugenzi wa Kampuni ya United Green na (kulia) Mshauri wa biashara Bw. Godfrey Lwakatare, kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Serikali Mtumba, Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.

Mkurugenzi wa kampuni ya United Green, Bw. Rod Bassett kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania akiwasilisha mapendekezo kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022. kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma pamoja na binafsi za Tanzania.

Sehemu ya menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo wakifatilia kwa makini mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na muwasilishaji (hayupo pichani) kwenye kikao kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya Mifugo na taasisi za Umma za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba,Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.

Menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa Mifugo  na wataalamu kutoka Idara ya Biashara za kimataifa kutoka ubalozi wa uingereza nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao, kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma na binafsi za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022.

SAUTI YETU WIKI HII

Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi ( sekta ya Uvuvi) Dk Rashid Tamatamah ( aliyesimama) akiwatambulisha wageni kutoka kampuni ya ALBACORA GROUP wa nchini Hispania ( waliokaa kulia) kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega. Kwenye kikao kilichofanyika  ofisi za wizara NBC, Dodoma, tarehe 20 Oktoba 2022. Lengo la ugeni huo ni kuona uwezekano wa wizara hiyo kuwasaidia kupata hekta elf 20 za ardhi kwa ajili ya kuwekeza kiwanda cha samaki jamii ya Tuna, kiwanda hicho kitachukua zaidi ya wafanyakazi elf 1 wakitanzania, na ( kushoto) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya bahari kuu Zanzibar  Dkt. Emmanuel Sweke.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki (katikati) na Naibu Waziri Abdallah Ulega (kushoto kwake) katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya kampuni ya ALBACORA GROUP kutoka Hispania ambao wamekuja nchini kwa lengo la kuona uwezekano wa wizara kuwasaidia kupata ardhi ya hekta elfu 20 kwa ajili ya kuwekeza kiwanda cha samaki jamii ya Tuna, kiwanda hicho kitachukua zaidi ya wafanyakazi watanzania elf moja. Tukio hili limefanyika katika Ofisi za Wizara zizopo NBC Mjini Dodoma leo tarehe 20/ 10/2022.

MTENDAJI MKUU WA WAKALA YA MAABARA YA VETERINARI, DKT. STELLA BITANYI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo (Dodoma).

 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari - Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi kuzungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari Maelezo (Dodoma).

Meneja wa Wakala ya Veterinari Tanzania (TVLA) kituo cha Dodoma Dkt. Japhet Nkangaga (kushoto) akifuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Stella Bitanyi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Oktoba 21,2022 alipokutana nao kuzungumzia majukumu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari - Maelezo (Dodoma) kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari - Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YASHIRIKI VIKAO VYA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kwa Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma akiongea na Viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Dkt. Emmanuel Sweke akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mamlaka hiyo ikiwemo mwenendo wa utoaji wa leseni za uvuvi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Sehemu ya Wataalamu  na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifuatilia wasilisho la utendaji kazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kwa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akieleza jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kwa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma akiongea na Viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati akifungua  kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akieleza jambo mbele ya Kamati ya Bajeti ya Bunge kuhusu Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 kwa kipindi cha Julai 1- Septemba 30, 2022 kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 22, 2022.

Sehemu ya Wataalamu  na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakichukua maelezo wakati wa kikao cha Kamati ya Bajeti ya Bunge kuhusu Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 kwa kipindi cha Julai 1- Septemba 30, 2022 kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 22, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma akiongea na Viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) kwa Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA), Dkt. Emmanuel Sweke akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mamlaka hiyo ikiwemo mwenendo wa utoaji wa leseni za uvuvi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 20, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Sehemu ya Wataalamu  na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifuatilia wasilisho la utendaji kazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kwa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akieleza jambo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kwa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI), Dkt. Ismael Kimirei akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dkt.Christine Ishengoma akiongea na Viongozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati akifungua  kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 21, 2022.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akieleza jambo mbele ya Kamati ya Bajeti ya Bunge kuhusu Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 kwa kipindi cha Julai 1- Septemba 30, 2022 kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 22, 2022.

Sehemu ya Wataalamu  na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakichukua maelezo wakati wa kikao cha Kamati ya Bajeti ya Bunge kuhusu Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 kwa kipindi cha Julai 1- Septemba 30, 2022 kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Oktoba 22, 2022.

SAUTI YETU WIKI HII

SAUTI YETU WIKI HII

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO TANZANIA (TALIRI)

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akifunga kikao cha kamati hiyo mara baada ya kupokea Taarifa ya Utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwenye kikao kilichofanyika bungeni Jijini Dodoma. (18.10.2022)

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akijibu baadhi ya hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji mara baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwenye kikao kilichofanyika bungeni Jijini Dodoma. (18.10.2022)

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Charles Mhina (aliyesimama) akiwasalimu Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kabla ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwenye Kamati hiyo bungeni Jijini Dodoma. (18.10.2022)

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba (kulia) akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Taasisi hiyo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji bungeni Jijini Dodoma. (18.10.2022)

Viongozi na Wataalam kutoka Sekta ya Mifugo wakifuatilia wasilisho la Taarifa ya Utendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji bungeni Jijini Dodoma. (18.10.2022)