Nav bar

Ijumaa, 28 Oktoba 2022

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UNITED GREEN KUTOKA UINGEREZA AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA - SEKTA YA MIFUGO

 


Mkurugenzi wa kampuni ya United Green, Bw. Rod Bassett kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania akiwasilisha mapendekezo kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022. kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma pamoja na binafsi za Tanzania.


Menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi upande wa Mifugo  na wataalamu kutoka Idara ya Biashara za kimataifa kutoka ubalozi wa uingereza nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao, kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya mifugo na taasisi za umma na binafsi za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba, Dodoma 21 Oktoba 2022.


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu sekta ya Mifugo, Dkt. Charles Mhina (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye kikao cha menejimenti ya wizara ya Mifugo na Uvuvi na wataalamu kutoka Ubalozi wa uingereza nchini Tanzania, (kushoto)  ni Mkurugenzi wa Kampuni ya United Green na (kulia) Mshauri wa biashara Bw. Godfrey Lwakatare, kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Serikali Mtumba, Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.


Sehemu ya menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo wakifatilia kwa makini mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na muwasilishaji (hayupo pichani) kwenye kikao kuhusu uwezekano na ushirikiano kati ya makampuni ya uingereza yanayofanya shughuli za sekta ya Mifugo na taasisi za Umma za Tanzania, kikao hicho kimefanyika katika ofisi za serikali Mtumba,Jijini Dodoma 21 Oktoba 2022.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni