Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2022

SERIKALI KUTOA MIKOPO KWA WAVUVI NA WAKUZAJI VIUMBE MAJI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuwapatia mitaji ili waweze kuboresha shughuli zao.   Waziri Ndaki ameyasema hayo leo (30.08.2022) kwenye hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya wizara ya mifugo na uvuvi (sekta ya uvuvi) na benki ya maendeleo ya kilimo tanzania – TADB, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza – Msalato Jijini Dodoma.   Mpango huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 07.01.2022 katika kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisisitiza kutumika kwa fursa zilizopo katika kukuza Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi na ukuzaji viumbe maji. Aidha, wakati akifunga Maonesho ya Sherehe za Wakulima (NANENANE), M...

WADAU TASNIA YA KUKU WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Picha
Na Mbaraka Kambona, Arusha Wadau wa tasnia ya kuku wamekutana kujadili changamoto zinazokabili mnyororo wa thamani wa tasnia ya kuku na kuweka vipaumbele vya uwekezaji kwa lengo la kuifanya tasnia hiyo kuwa na mchango mkubwa zaidi katika pato la taifa. Wadau hao kutoka serikalini na sekta binafsi walikutana jijini Arusha Agosti 29, 2022. Akifungua mkutano huo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki alisema pamoja na jitihada zinazoendelea kufanywa kukuza tasnia ya kuku bado tasnia hiyo inaonekana ni ndogo, hivyo aliwataka wadau hao kujadili kwa kina ni namna gani wafanye ili tasnia hiyo iwe na mchango unaotarajiwa. "Kwa hiyo taarifa ya mnyororo wa thamani wa tasnia ya kuku mtakayoijadili leo mtaweza kuwa na majibu ya changamoto zilizopo katika kuifanya tasnia hii inakwama hasa katika eneo la afya ya kuku, biashara na masoko na kutafutia ufumbuzi changamoto hizo", alisema Aliongeza kwa kusema kuwa pamoja na tasnia hiyo kuendelea kutoa mchango wake katika lishe na kipat...

SEKTA YA MIFUGO YAFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMPUNI MAKUBWA YA NCHINI UINGEREZA

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Mifugo amesema kuwa wameanza kufanya mazungumzo na Makampuni makubwa yanayojishughulisha na shughuli za mifugo ya nchini Uingereza.   Katibu Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo (29.08.2022) baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliowashirikisha Viongozi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, baadhi ya Wadau wa Sekta ya Mifugo waliopo nchini Uingereza pamoja na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Sekta ya Mifugo, mkutano ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Wizara uliyopo kwenye Mji wa Serikali – Mtumba Jijini Dodoma.   Mkutano huo ulijadili namna wadau hao kutoka nchini Uingereza wanavyoweza kuja kushirikiana na wadau wa Sekta ya Mifugo hapa nchini hasa wafuga ili kuikuza zaidi sekta hiyo.   Lengo hasa la mkutano huo ni kuona ni namna gani makampuni hayo yanaweza kusaidia kuimarisha mfumo wa ufugaji nchini kwa kutumia teknolojia rahisi za malisho ya mifugo, mbegu za mif...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

LITA KIKULULA YATAKIWA KUENDELEA KUSAIDIA WANANCHI

Picha
Na Mbaraka Kambona,  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki ameipongeza Wakala ya Mafunzo ya Mifugo, Kampasi ya Kikulula (LITA-Kikulula) iliyopo Wilayani Karagwe Mkoani Kagera kwa kazi nzuri ya kuwawezesha wananchi ujuzi wa kufuga kisasa huku akiwataka kuendelea kuwasaidia wananchi kufanya ufugaji wa kisasa, wenye tija zaidi kwao na Taifa kwa ujumla. Waziri Ndaki alitoa kauli hiyo Agosti 26, 2022 wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kampasi hiyo kwa lengo la kukagua shughuli wanazozifanya. "Napenda kuipongeza Kampasi hii ya LITA Kikulula kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kazi zao, ukijaribu kuangalia rasilimali walizonazo na kile wanachokitoa utaona kwamba ni juhudi kubwa wanafanya ili kuwa na matokeo haya wanayoyapata," alisema Alisema kuwa kampasi hiyo imeendelea kupata matokea hayo kwa sababu wanafundisha kwa vitendo zaidi kuliko maneno na ndio maana alipokutana na wanafunzi wa katika kampasi hiyo walimueleza Waziri huyo kuwa kutokana na Mafunzo wanayoyapata w...

SERIKALI KUSHIRIKISHA WADAU BEI ELEKEZI ZA MIFUGO

Picha
Na Mbaraka Kambona, Chato Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kushirikisha wadau wa sekta ya mifugo kupanga bei elekezi za kuuzia mifugo katika minada ili kuwawezesha wafugaji na  wafanyabiashara kuuza mifugo yao kwa bei ambayo wao watakuwa wameshiriki kuipanga. Alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnada wa Kimataifa  wa Buzirayombo unaojengwa Wilayani Chato, Mkoani Geita Agosti 26, 2022. Alisema suala la kuwa na bei elekezi, Serikali inalifanyia kazi na tayari Wataalam walishaandaa na hatua iliyopo sasa ni ya kuwashirikisha wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo ili kwa pamoja waweze kukubaliana na kuja na bei ambayo itakuwa imeridhiwa na pande zote. "Bei elekezi ikitoka ndio itakuwa mahali pa kuanzia na kwenda juu, hivyo tunalifanyia kazi suala hilo na muda sio mrefu tutato muelekeo wa jambo hilo", alisema Aliongeza kwa kusema kuwa sambamba na bei elekezi Serikali inataka sasa mifugo yote ...

WAWEKEZAJI WAZAWA WAHIMIZWA KUWEKEZA SEKTA YA MIFUGO

Picha
Na Mbaraka Kambona, Kagera Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewahimiza wawekeza kutoka Sekta binafsi nchini kuwekeza katika sekta ya mifugo kwa sababu kuna fursa kubwa ya kukuza mitaji yao na kupata faida. Alitoa wito huo alipotembelea na kukagua maendeleo ya kiwanda cha kuchakata maziwa na chakula cha mifugo cha Kahama Fresh kilichopo Wilayani Karagwe, Mkoani Kagera Agosti 25, 2022.  Waziri Ndaki aliwahimiza wawekezaji wa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya mifugo nchini kwa sababu inawezekana  akitolea mfano muwekezaji huyo wa Kahama Fresh ambaye alianza uwekezaji katika shamba alilopewa na serikali na mpaka sasa amefungua kiwanda cha kuchakata maziwa na chakula cha mifugo. "Niseme tu kwamba sisi Wizara ya Mifugo tuko tayari kumuunga mkono mwekezaji yeyote atakayeweza kufanya uwekezaji mahiri kama alivyofanya Kahama Fresh ili  shughuli ya ufugaji iwe ya  kibiashara zaidi na kuleta tija kwao binafsi na Taifa kwa ujumla," alisema Aliongeza kwa kusem...

MPANGO WA KUWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI WAIVA

Picha
  Na Mbaraka Kambona, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa vituo atamizi vinne kwa ajili ya kuwafundisha vijana unenepeshaji wa mifugo ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia Sekta ya Mifugo. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki Agosti 24, 2022 wakati akitoa taarifa kwa umma ya kuwataka vijana kujitokeza kuomba nafasi za kujiunga katika Vituo Atamizi vilivyoandaliwa Mkoani Tanga, Mwanza na Kagera. Alisema Mhe. Rais Samia anataka kuona vijana wanawezeshwa kujiajiri kupitia Sekta ya Mifugo kwani fursa zilizopo katika sekta hiyo ni nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa taifa. Aliongeza kwa kusema kuwa wanaanzisha vituo hivyo kuwafunza vijana kufanya ufugaji kwa njia ya vitendo ili waweze kutumia ujuzi huo kujiajiri na kujiongezea kipato. “Hawa vijana 240 watakaokuwa katika vituo hivyo vilivyoandaliwa wataelimishwa namna ya kufanya ufugaji wa kibiashara ili waweze kusaidia kuwabadilisha wafugaji wengin...

​ULEGA: VIJANA CHANGAMKIENI FURSA UCHUMI WA BULUU

Picha
Na Mbaraka Kambona, Mwanza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahimiza vijana wa Kanda ya Ziwa Viktoria kufuga samaki ili kujiongezea kipato na kuongeza fursa za ajira nchini. Waziri Ulega alitoa wito huo kwa nyakati tofauti akiwa ziarani katika Wilaya za Ukerewe na Ilemela zilizopo mkoani Mwanza Agosti 20, 2022. Alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kutumia fursa za uchumi wa buluu zilizopo ndani ya Ziwa Viktoria kuwawezesha vijana kufuga samaki kwa kutumia vizimba na kuuza samaki hao ndani na nje ya nchi ili kujiongezea kipato. "Rais Samia ametoa bilioni 20 kwa ajili ya kuwezesha vijana kufuga samaki katika vizimba, hivyo ni wakati sasa wa kujipanga ili pesa hizo zitakapokuja tuweze kuzitumia vizuri kufanya uzalishaji wa samaki kwa wingi ili tuweze kuuza na kupata kipato", alisema Aliongeza kwa kusema kuwa samaki aina ya sato wanahitajika sana ndani na nje ya nchi, uhitaji ni mkubwa hivyo vijana wajipange vizuri ili waweze kutumia furs...

WAZIRI NDAKI ATAKA AGIZO LA RAIS SAMIA JUU YA MAENEO YA WAFUGAJI KUTEKELEZWA

Picha
Na. Edward Kondela   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) amezitaka halmashauri na mamlaka za serikali za mikoa kuhakikisha zinatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji ili kukuza sekta hiyo na kuepusha migogoro ya matumizi bora ya ardhi. Waziri Ndaki amebainisha hayo (19.08.2022) alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro na kuzungumza na wakulima na wafugaji katika vijiji vya Tanga na Njiwa, ambapo amesema serikali ina nia nzuri ya kuendeleza Sekta ya Mifugo na kuzitaka halmashauri hizo na mamlaka za serikali za mikoa kutekeleza agizo hilo huku akiwataka wafugaji kutolisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima. Ameongeza kuwa serikali pia imeelekeza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho kuanzia ngazi ya kijiji ambayo hayajasajiliwa, yanatakiwa kutambuliwa rasmi na kusajiliwa pamoja na kulindwa na kuhakikisha yanatumika kama ilivyopangwa kwa aji...

SPIKA MSTAAFU MSEKWA APONGEZA UCHUMI WA BULUU WA SERIKALI YA RAIS SAMIA

Picha
Na Mbaraka Kambona, Mwanza Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Pius Msekwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuwezesha vijana kufuga samaki ili wanufaike kupitia uchumi wa buluu. Mzee Msekwa alibainisha hayo alipotembelewa  nyumbani kwake Wilayani Ukerewe na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa  ziara yake aliyoifanya Wilayani humo, Mkoani Mwanza Agosti 19, 2022. Alisema kuwa mambo ambayo yanafanywa na Serikali ya awamu ya sita hususan ya kuwezesha vijana kujiajiri ni mambo ambayo Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alitamani sana kuyafanya na hivyo kama angekuwa hai mpaka leo angefurahi sana. "Haya yote uliyoyasema Mwl. Nyerere alitamani kuyafanya wakati wa uhai wake, kama angekuwepo leo angefurahi sana kwa sababu yale yote aliyoyataka kuyafanya Rais Samia anayaendeleza kwa kasi kubwa, hongereni sana",  alisema Awali, akitoa taarifa ya fupi kuh...

MKUTANO NA WAWEKEZAJI WA KAMPUNI YA BLUE CHELE CHELE KUTOKA NCHI YA SHELISHELI

Picha
  Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Magese Bulayi (katikati) akiongoza mkutano na wawekezaji wa Kampuni ya BLUE CHELE CHELE kutoka nchi ya Shelisheli hawapo pichani. Lengo la mkutano huo ni kujadili na kukubaliana maeneo ambayo wanaweza kuwekeza katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari  na Mwambao wa Bahari ya Hindi katika  Sekta ya Uvuvi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Viumbe Maji Bw. Nazaeli Madala na Kushoto ni Muwakilishi kutoka Mamlaka ya Uvuvu wa Bahari Kuu (DSFA) BW. Peter Shunula. Mkutano huo umefanyika MVUVI HOUSE - Dsm,  (18.08.2022) Balozi wa Heshima kutoka Jamhuri ya Shelisheli Bi. Màryvonne Pool (kushoto) akiongoza msafara huo wa wawekezaji kutoka SheliSheli amefuatana na Muwekezaji kutoka  Kampuni ya BLUE CHELE CHELE Bw. Danny Lowman (katikati)na Mshauri Muelekezi Bi. Sheryl Vangadasamy katika mkutano huo. (18.08.2022) Kikao na Wawekezaji kutoka SheliSheli kimehudhuriwa na Wataalamu kutoka Idara ya Uvuvi (HQ), TAFIRI, MPRU, DSFA, TAFICO na Maafisa Wafawid...