Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa serikali imeandaa mpango wa kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuwapatia mitaji ili waweze kuboresha shughuli zao.
Waziri
Ndaki ameyasema hayo leo (30.08.2022) kwenye hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za
uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya wizara ya mifugo na uvuvi (sekta ya
uvuvi) na benki ya maendeleo ya kilimo tanzania – TADB, hafla iliyofanyika
kwenye ukumbi wa Mzee uliopo katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza – Msalato
Jijini Dodoma.
Mpango huu ni sehemu ya
utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzani katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 07.01.2022
katika kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisisitiza
kutumika kwa fursa zilizopo katika kukuza Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi na
ukuzaji viumbe maji. Aidha, wakati akifunga Maonesho ya Sherehe za Wakulima
(NANENANE), Mheshimiwa Rais aliagiza Wizara kuhakikisha kuwa uzalishaji wa
Samaki unaongezeka kutoka tani 497,567 na kufikia tani 600,000 ifikapo mwaka
2025.
Katika utekelezaji wa
maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeandaa Mpango wa
kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa
vyama vya ushirika, vikundi vya wavuvi, wakuzaji viumbe maji, wavuvi binafsi na
makampuni ya wavuvi. Mikopo hiyo itahusisha zana za kisasa za uvuvi ikiwemo
boti, nyavu, injini, vizimba,
vifaranga vya samaki, chakula cha samaki na pembejeo za ukulima wa mwani.
Waziri
Ndaki ametoa wito kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji kuchangamkia fursa hiyo ya
mikopo ili iweze kuwanufaisha. Aidha, amezisihi Halmashauri katika
maeneo ya mradi kwenda kuwahamasisha wananchi wake ili waweze kuitumia kuitumia
fursa hii ipasavyo.
Aidha, amemshukuru Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kuendeleza
Sekta ya Uvuvi, fedha ambazo zipo katika bajeti ya mwaka 2022/2023. Waziri
Ndaki amesema endapo zikitumika vizuri upo uwezekano mwaka ujao wa fedha fedha
hizo zikaongezeka.
Waziri Ndaki amesema kama
viongozi watahakikisha wanawasimamia wataalam wa Wizara kwa kuwa mradi huu
unatakiwa kutakelezwa kwa muda maalum, hivyo ifikapo Juni 30, 2023 utekelezaji
wa mradi huu uwe umekamilika.
Naye Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa kasi ya utoaji mikopo kwa wavuvi
kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ni ndogo, kwani mahitaji ya watanzani,
kasi ya kuwafiki na urahisi wa upataji mikopo bado ni mdogo. Hivyo TADB inayo
kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha kwamba mikopo inafika kwa walengwa, kwani
watu wengi wamehangaika kupata mikopo hasa wavuvi wadogo na kusababisha kukata
tamaa na kuacha kufanya shughuli za uvuvi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma amesema kuwa
Kamati imefurahishwa sana na mpango wa serikali wa kutoa mikopo isiyo na riba
inayokwenda kuwasaidia wavuvi na wakuzaji viumbe maji. Mradi huu utakwenda
kusaidia kuongeza uzalishaji wa samaki utakaokwenda kukidhi mahitaji makubwa
yaliyopo.
Katibu Mkuu anayesimamia Sekta
ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa boti hizo zina urefu wa
mita 7 hadi 14 zikiwa na injini zenye uwezo wa nguvu za farasi 9.9
hadi 60. Pia boti hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba wavuvi 6 – 20,
kubeba Samaki tani 1.5, mtambo wa kufuatilia/kutambua uwepo wa Samaki
(Fish finder), kifaa cha kuongoza boti (GPS), vifaa vya kuokolea Maisha na zana
za uvuvi zikijumuisha mishipi na nyavu. Jumla ya shilingi Bilioni 11.5 zimetengwa kwa ajili ya kukopeshwa na mkopo
huo utalipwa kwa muda wa miaka mitano (5) bila Riba.
Wizara
pia itatoa mkopo kwa Wafugaji Samaki kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kujenga
jumla ya vizimba 831 ambapo kila kizimba kimoja kitakuwa na ukubwa wa mita za
ujazo 144 M3 – 256 M3. Vilevile, itatoa jumla ya vifaranga 4,080,000 na chakula cha Samaki
tani 3,482.5.
Aidha,
mkataba huo uliosainiwa leo utahusisha wakulima wa mwani ambapo jumla ya
wakulima 821 watakopeshwa kamba 108,372, tai tai 7,152,552
pamoja na mbegu za mwani. Kwa ujumla kiasi cha shilingi Bilioni 21
zitatumika kwa ajili ya vizimba na zao la mwani.
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania,
Frank Nyabudenge amesema kuwa benki hiyo ni taasisi ya kifedha ambayo ni benki
ya serikali iliyojikita kwenye sekta ya kilimo. Moja ya malengo makubwa ya
kuanzishwa kwake ni kuchangia utoshelevu wa chakula na usalama endelevu wa
chakula nchini ambapo ni pamoja na utoaji lishe bora.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Tanzania, Frank Nyabudenge (wa pili kulia wakisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). (30.08.2022)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akitoa salam wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambapo amesema kuwa kasi ya utoaji mikopo kwa wavuvi kupitia TADB ni ndogo, kwani mahitaji ya watanzani, kasi ya kuwafiki na urahisi wa upataji mikopo bado ni mdogo, hivyo TADB inayo kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha kwamba mikopo inawafikia walengwa kwa wakati. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30,08,2022)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb) akitoa salam za kamati wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) amesema kuwa Kamati imefurahishwa sana na mradi huu wa kuwakopesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kwa kuwa utawasaidia kuongeza uzalisha na hivyo kuongeza upatikanaji wa samaki. Aidha, amesema kuwa Kamati itaendelea kuisimamia Wizara ili kuhakikisha maendeleo kwenye Sekta ya Uvuvi yanapatikana. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) amesema kuwa jumla ya wakulima 821 watakopeshwa kamba 108,372, tai tai 7,152,552 pamoja na mbegu za mwani. Kwa ujumla kiasi cha shilingi Bilioni 21 zitatumika kwa ajili ya vizimba na zao la mwani. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Naibu Katibu Mkuu, OR TAMISEMI (Afya), Dkt. Grace Magembe akitoa salam wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) amemuhakikishia Waziri kuwa TAMISEMI itashiriki kikamilifu kwenye mkakati huo kwa kuwa tayari wanayo mifumo ambayo ilikuwa ikitumika kwenye utoaji wa fedha. Hivyo watashirikiana na wataalam kutoka Sekta ya Uvuvi kuangalia ni wapi wanafanya vizuri na kama kutakuwa na changamoto ziweze kutatuliwa ili mradi huu uweze kuleta tija na matokeo yaliyotarajiwa. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Frank Nyabudenge akitoa salam za TADB wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) amesema kuwa watahakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa nakutoa matokeo chanya ya kuongeza mazao yatokanayo na uvuvi. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Frank Nyabudenge akitoa salam za TADB wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) amesema kuwa watahakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa nakutoa matokeo chanya ya kuongeza mazao yatokanayo na uvuvi. Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Tanzania, Frank Nyabudenge (kulia) wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo. (30.08.2022)
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitenge wa Wizara hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah na Kamati ya maandalizi mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ununuzi wa boti za Uvuvi na vizimba vya kufugia samaki kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mzee uliopo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza - Msalato Jijini Dodoma. (30.08.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni