Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Bw. Tixon Nzunda amesema mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirishia mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi utawezesha kurejesha mrejesho wa haraka na kwa wakati.
Bw. Nzunda ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya mfumo huo kwa wataalamu wa sekta ya mifugo wa mkoa wa Mbeya leo 14 June, 2022.
Amesema, Kwa kuandaa mfumo huo utakwenda kupunguza vikwazo vya wafanyabiashara, utakwenda kuvutia uwekezaji kwenye sekta pia utakwenda kuongeza tija ya uzalishaji katika sekta ya mifugo,
"Tunajua mfumo baadhi ya michakato ambayo mlikuwa mmeizoea haitakuwepo kwahiyo msikumbatie kwamba mlikuwa mmezoea hivi lazima iwe hivi" amesema Nzunda.
Amesema kupitia mfumo huu mfanyabiashara wa ndani ya nchi, wa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, mfanyabiashara nje ya nchi na nje ya ukanda wetu wataweza kufanya biashara huru kwenye sekta ya Mifugo popote walipo.
Aidha, amesema mifumo hii itawezesha ununuzi, utoaji wa vibali vya mazao ya mifugo, hivvyo mfumo utakwenda kujenga misingi ya usikivu na uwajibikaji wa Umma.
pi ameongezea kwa kuwaasa wataalamu wa sekta ya mifugo wasitumie nafasi hiyo kuhujumu mfumo kwa sababu ya mazoea waliyokuwa wamezoea kulinda urasimu na kutengeneza mazingira yoyote yatakayokwamisha uboreshaji na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu haya.
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Baltazar Kibola akiongea na wataalamu wa sekta ya Mifugo wa mkoa wa Mbeya walioshiriki mafunzo ya mfumo mpya wa kielektroniki wa Usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirishia mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi uitwao "Mifugo Integrated Management Information System"(MIMIS) (hawapo pichani) wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe Hotel, Jijini Mbeya, 14 June 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni