Sekta za Mifugo za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ) kupitia Makatibu wake wakuu wamekutana na kupitia utekelezaji wa
maazimo yaliyowekwa ili kuendeleza sekta hiyo.
Akifungua kikao hicho
leo (13.06.2022) Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo (SMT), Dkt. Charles Mhina
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma amesema kuwa serikali
ina lengo la kuhakikisha sekta ya mifugo inakua na kuongeza mchango wake kwenye
pato la taifa.
Dkt. Mhina amesema
kuwa katika kikao kilichopita yapo maazimio yaliyowekwa ambayo yanapitiwa
utekelezaji wake, lengo likiwa ni kuhakikisha sekta ya mifugo inawanufaisha
wafugaji na wadau walio kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza mchango wa sekta
kwenye pato la taifa.
“Vikao hivyo vya
ushirikiano wa kuendeleza Sekta ya Mifugo vinajadili maendeleo ya sekta katika
udhibiti wa magonjwa yanayovuka mipaka, uboreshaji wa kosaafu za mifugo, masoko
ya mifugo na mazao yake na kuona ni changamoto zipi zinazoikabili sekta ya
mifugo katika pande zote mbili za Muungano ili kuzitatua,” alisema
Dkt. Mhina amesema
kuwa kikao hicho kimepitia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa kwenye kikao
kilichopita na kuona utekelezaji uliofanyika kwenye baadhi ya maeneo, lakini
pia yapo maeneo mapya ambayo wamebaini kuwepo kwa changamoto nyingine ambazo
pia tayari wameshaziwekea maazimio ya utekelezaji, lengo kuu ni kuhakikisha
sekta inakua kwa pande zote mbili za SMT na SMZ.
Kwa upande wake mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo (SMZ), Bi. Asha Zahran
amesema kuwa kupitia vikao hivyo tayari wameshaanza kuona mafanikio yake kwani
wapo wataalam kutoka Zanzibar ambao wamepata mafunzo ya kuhimilisha Ng’ombe
kupitia kituo cha NIC, mbegu bora za ng’ombe, kilimo cha malisho pamoja na
masuala ya udhibiti wa magonjwa kutoka SMT. Hivyo ushirikiano huu ukiendelea
utawezesha sekta ya mifugo kuimarika kwa pande zote za Muungano.
Naye mwakilishi kutoka
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Bw. Allan Bendera alisema kuwa Wizara
inaendelea kuhakikisha changamoto zinazohusu Muungano zinatatuliwa ili
kudumisha muungano kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla. Hivyo kwa upande wa Sekta
ya Mifugo changamoto zilizojitokeza zitaendelea kufanyiwa kazi kwa pande zote
za Muungano lengo likiwa ni kuwasaidia wafugaji waweze kuongeza kipato na
kuongeza kipato cha Sekta ya Mifugo kwenye pato la Taifa.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Charles Mhina (kushoto) akifungua kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo aliwasisitiza wajumbe kujadili kwa kina changamoto zinazoikabili Sekta ya Mifugo na kuzitafutia utatuzi wake ili kuendeleza sekta hiyo. Kulia ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Bi. Asha Zahran. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo (SMZ), Bi. Asha Zahran akifunga kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo amewasihi wajumbe kuhakikisha wanayafanyia kazi maazimio yote yalioafikiwa kwa wakati ili kuleta maendeleo kwenye Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga akichangia mada wakati wa kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichojadili maendeleo ya Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angelo Mwillawa akifafanua jambo wakati wa kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichojadili maendeleo ya Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar, Kanali Ali Hamad akizungumza wakati wa kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichojadili maendeleo ya Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar, Kanali Ali Hamad akizungumza wakati wa kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichojadili maendeleo ya Sekta ya Mifugo. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Washiriki wa kikao cha Ushirikiano kati ya Serikali ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichojadili maendeleo ya Sekta ya Mifugo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao hicho. Kikao hicho kimefanyike kwenye ukumbi wa ofisi ya Jeshi la Zimamoto Jijini Dodoma. (13.06.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni