Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa
vilivyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa
Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ambao umechangia Shilingi Bilioni 1.1 kwa
ajili ya kununua malori na vifaa hivyo. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja
vya kiwanda cha kusindika maziwa Tanga Fresh jijini Tanga, ambapo amesisitiza
ufugaji wa ng'ombe bora wa maziwa ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa
maziwa nchini. (29.01.2021)
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Michael akizungumza wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya malori na vifaa vya maziwa vilivyotolewa na shirika la
kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa
Tanzania (TMPP), iliyofanyika katika viwanja vya kiwanda cha kusindika maziwa
Tanga Fresh jijini Tanga, ambapo amesema wizara inaweka jitihada mbalimbali za
kuhakikisha upatikanaji wa mbegu za ng'ombe bora wa maziwa nchini. (29.01.2021)
Mkurugenzi wa Mradi wa Usindikaji wa
Maziwa Tanzania (TMPP), ulio chini ya shirika la kimataifa la Heifer
International Bw. Mark Tsoxo akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya
malori na vifaa vya maziwa vilivyotolewa na mradi huo kama mchango wake kwenye
tasnia ya maziwa nchini ambapo ameshukuru ushirikiano uliopo kati ya serikali
na sekta binafsi. (29.01.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi malori manne yaliyotolewa na
shirika la kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa
Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni mchango wake katika tasnia ya maziwa ambapo
malori hayo ya kubebea maziwa yametolewa kwa wadau wa tasnia ya maziwa nchini
vikiwemo viwanda vitatu vya kuchakata maziwa (ASAS, Kilimanjaro Fresh na Nronga)
na Chama Kikuu cha Ushirika wa Wafugaji Mkoa wa Tanga (TDCU). Hafla hiyo fupi
imefanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh
kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki akiwa kwenye moja ya malori ya kubebea maziwa yaliyotolewa na shirika la
kimataifa la Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa
Tanzania (TMPP), ikiwa ni mchango wake katika tasnia ya maziwa nchini kwenye
hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga
Fresh kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki akimkabidhi Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Bw. Noel Byamungu moja
ya matanki ya kubebea maziwa yaliyotolewa na shirika la kimataifa la Heifer
International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni
mchango wake katika tasnia ya maziwa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika
viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga.
(29.01.2021)
Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na baadhi ya wadau wa tasnia ya maziwa nchini
waliokabidhiwa malori na vifaa vya maziwa na shirika la kimataifa la Heifer
International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP), ikiwa ni
sehemu ya mchango wake katika tasnia ya maziwa ambapo hafla hiyo fupi
imefanyika katika viwanja vya kiwanda cha kuchakata maziwa Tanga Fresh
kilichopo jijini Tanga. (29.01.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella mara baada ya Waziri
Ndaki kufika katika ofisi za mkuu wa mkoa kabla ya kushiriki katika hafla fupi
ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa yaliyotolewa na shirika la kimataifa la
Heifer International kupitia Mradi wa Usindikaji wa Maziwa Tanzania (TMPP),
ambapo Mhe. Shigella amemuarifu Waziri Ndaki juu ya changamoto ya uwepo wa
mitamba ya kutosha Mkoani Tanga kwa ajili ya kuzalisha maziwa mengi.
(29.01.2021)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki (wa kwanza kulia), wataalam kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Bodi ya Maziwa na wadau wengine wa sekta ya mifugo
wakifuatilia somo la uboreshaji ng'ombe wa maziwa linalotolewa na Meneja
wa shamba la mifugo la Mruwazi lililopo
Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga Bw.
William Mgunya muda huu baada ya timu hiyo kufika shambani hapo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki (wa kwanza kushoto) akipokea
maelezo kuhusu aina ya ng'ombe aliowakuta kwenye shamba la mifugo la Mruwazi
lililopo Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga yanayotolewa na Meneja wa shamba
hilo Bw. William Mgunya (kushoto kwake)
muda huu (30.01.2021) baada ya kufika shambani hapo. Wengine pichani ni baadhi
ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bodi ya Maziwa na Shirika la kimataifa
la Heifer.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni