Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akieleza kwa ufupi umuhimu
wa Kiwanda cha Ace Leather Tanzania Ltd katika kuleta maendeleo ya Sekta ya
Mifugo hususan katika tasnia ya ngozi mapema leo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda
hicho uliofanyika Mkoani Morogoro Februari 12, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
Kiwanda cha kuchakata Ngozi cha Ace Leather Tanzania Ltd kilichopo Kihonda,
Mkoani Morogoro Februari 12, 2021. Kulia kwake ni Mmiliki wa Kiwanda hicho,
Rostam Aziz. Wa kwanza kulia, mstari wa nyuma ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel. Wengine ni Viongozi Wakuu wa
Serikali na baadhi ya wamiliki wa kiwanda hicho.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akimueleza jambo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani
Jafo (katikati) walipokutana katika uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata Ngozi cha
Ace Leather Tanzania Ltd uliofanyika Mkoani Morogoro leo Februari 12, 2021. Wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Morogoro Mjini, Georgina
Matagi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni