Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akifanyia majaribio ya moja ya
vifaa vilivyopo kwenye maabara za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini
(LITA) Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha ambazo zimekarabatiwa majengo na
kuwekewa vifaa vya kisasa kwa ushirikiano kati ya nchi ya Poland na LITA.
(01.12.2020)
Baadhi ya vifaa vilivyopo
katika moja ya maabara kati ya mbili za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo
nchini (LITA) Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha, ambazo zitatumika kwa ajili ya
kufanya utafiti wa kuchunguza wadudu wanaoonekana kwa macho ambao wanaathiri
mifugo pamoja na kuchunguza vimelea vya magonjwa ambavyo havionekani kwa macho.
(01.12.2020)
Muonekano wa nje wa jengo la
maabara za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Kampasi ya
Tengeru, mkoani Arusha ambazo zimegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 200 ikiwa
ni ukarabati wa majengo na vifaa kwa ushirikiano kati ya nchi ya Poland na
LITA. (01.12.2020)
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA), Dkt. Pius Mwambene akizungumza kwenye
hafla ya uzinduzi wa maabara za LITA Kampasi ya Tengeru Mkoani Arusha, ambapo
amesema maabara hizo zitatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi ili
waweze kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo nchini na kutoa tiba sahihi.
(01.12.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uzinduzi wa
maabara za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Kampasi ya
Tengeru, Mkoani Arusha ambapo ametaka maabara hizo zitumike vizuri ili
kuhakikisha wanafunzi wa kampasi hiyo wanapata elimu bora itakayowezesha
sayansi katika kukuza Sekta ya Mifugo nchini. (01.12.2020)
Balozi wa Poland nchini
Tanzania, Mhe. Krzysztof Buzalski akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara za
Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Kampasi ya Tengeru, Mkoani
Arusha ambapo nchini yake imetoa ufadhili katika kufanyia ukarabati majengo ya
maabara na kutoa vitendea kazi, amesema Poland itaendelea kuijengea uwezo LITA
katika eneo la utafiti na maabara. (01.12.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na balozi wa Poland hapa nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski
(aliyekaa wa pili kutoka kushoto) pamoja na viongozi wa Wakala ya Vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) na wafanyakazi wa LITA Kampasi ya Tengeru,
Mkoani Arusha baada ya uzinduzi wa maabara za LITA katika kampasi hiyo.
(01.12.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na balozi wa Poland hapa nchini Mhe. Krzysztof Buzalski
(aliyekaa wa pili kutoka kushoto) pamoja na maafisa kutoka Poland na viongozi
wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA), baada ya uzinduzi wa
maabara za LITA Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha zilizogharimu zaidi ya
Shilingi Milioni 200 fedha ambazo zimetolewa na serikali ya Poland pamoja na
LITA. (01.12.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa maelekezo kwa Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Dkt. Pius Mwambene
(wa kwanza kushoto) juu ya umuhimu wa malisho bora ya mifugo mara baada ya
kutembelea shamba la malisho lililopo LITA Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha
ambalo pia linaendeshwa kwa ushirikiano kati ya nchi ya Poland na LITA.
(01.12.2020)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa katikati) akiwa kwenye
picha ya pamoja na balozi wa Poland hapa nchini Mhe. Krzysztof Buzalski
(aliyekaa wa pili kutoka kushoto), viongozi wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya
Mifugo nchini (LITA), pamoja na baadhi ya wanafunzi wa LITA Kampasi ya Tengeru,
Mkoani Arusha baada ya uzinduzi wa maabara za LITA katika kampasi hiyo.
(01.12.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni