Wataalamu wa Mifugo wametakiwa kutumia taaluma zao na kushiriki kikamilifu katika kubuni mbinu za kisasa za kuinua viwango vya minyororo ya thamani ya mazao ya Mifugo na Uvuvi ili kuleta tija na kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amos Zephania alisema hayo alipokuwa akifungua
Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na
Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa
Mifugo Tanzania linalofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba 2- 4, 2020.
Zephania alisema kuwa
Serikali imedhamiria kuanzisha na kuendeleza viwanda mbalimbali hususani vya
uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo ambavyo ni msingi wa
maendeleo endelevu.
“Serikali inatambua kuwa
maendeleo ya viwanda hapa nchini yatachagiza upatikanaji wa bidhaa muhimu na
bora kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi jambo ambalo litainua ubora na
viwango vya maisha ya wananchi, kujenga uchumi imara na kukuza uchumi wa Taifa unaoweza
kuhimili ushindani wa kikanda na kimataifa,” alisema Zephania
Aliendelea kusema kuwa ni
wazi kwamba mifumo ya uzalishaji wa mifugo na uvuvi katika nchi yetu imeegemea
zaidi katika uzalishaji kwa mifumo ya asili ambapo wazalishaji wengi ni
wafugaji na wavuvi wadogo wadogo.
Aliongeza kuwa mifugo mingi
iliyopo bado ni ya asili ambayo tija
katika uzalishaji wake hairidhishi huku akisema kuwa ngómbe wengi wa asili wana uzito mdogo wa
kati ya kilo 200 hadi 350 ambao
hupelekea kutoa maziwa kidogo na nyama
kidogo ambayo haizidi wastani wa kilo 175.
Kufuatia hali hiyo, Zephania
alisema kuwa Wataalamu wa Mifugo wanajukumu la kufanya kuleta mabadiliko katika
mifumo ili kuongeza ufanisi na tija ya uzalishaji kwa kutumia sayansi na
teknolojia za kisasa huku akiwasisitiza
kuwasaidia wafugaji waweze kuongeza ubora wa uzalishaji ili mali ghafi za uhakika ziweze kupatikana kwa
matumizi ya viwanda vya kusindika mazao
ya mifugo na uvuvi.
“Huu ni wakati mwafaka wa
kufanya mapinduzi makubwa katika minyororo ya thamani ya mifugo na samaki ili
kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda tunaouzungumzia kwa sababu mahitaji ya
lishe ya protini inayotokana na mifugo yanatarajiwa kuongezeka kwa kiasi
kikubwa katika miaka 20 ijayo kutokana na ongezeko la idadi ya watu, kukua kwa
miji na kuongezeka kwa kipato cha watu,” aliongeza Zephania
“Hivyo ni lazima uzalishaji wa mifugo na samaki uboreshwe ili kukidhi mahitaji haya,
wahimizeni wafugaji na wazalishaji kuwekeza katika teknolojia na vitendea kazi
sahihi vitakavyowaongezea uzalishaji mashambani mwao na kuwawezesha kufikia
masoko kwa ufanisi zaidi,”alifafanua Zephania
Aidha, Zephania aliwahimiza
wataalamu hao kuendelea kuimarisha afya za mifugo, usimamizi wa mifumo bora ya
uzalishaji na kutoa huduma za ugani kwa wakati sambamba na uboreshaji wa
miundombinu ya masoko ikiwemo uhifadhi, usafirishaji na usambazaji wa mazao hayo
huku akisema kuwa mazao ya mifugo na uvuvi yanaharibika upesi yasipotunzwa na
kuhifadhiwa ipasavyo.
Naye, Katibu Tawala wa Mkoa
wa Dodoma, Maduka Kessy alisema kuwa jukumu la Wataalamu hao ni kuinua tija na
faida kwa wafugaji wanaoshiriki katika uwekezaji kwenye mnyororo mzima wa
thamani.
Kessy aliongeza kuwa Mkoa wa
Dodoma una zaidi ya Kaya Mia nne na Hamsini Elfu (450,000) na kati ya kaya hizo
Asilimia 44 ni wafugaji na ndio wenye kipato cha chini na maendeleo yao ni
duni, hivyo kuna haja ya kuwaendeleza ili waweze kunufaika na mifugo yao.
“Dodoma ni miongoni mwa mikoa
inayoongoza kwa kuwa na mifugo mingi, mpaka sasa takwimu zinaonesha tuna
ng’ombe milioni 1.8 lakini mnyororo wa thamani kwa mifugo hiyo ni mfupi sana,
hivyo kuwepo kwenu hapa leo ni faraja ya kwamba mtakuwa chachu ya mabadiliko
kwa wafugaji wetu ili waweze kufaidika na mifugo yao,” alisema Kessy
Kessy aliendelea kusema kuwa mfumo wa ufugaji kwa wananchi wengi umepitwa na wakati huku akiongeza kuwa kasi ya ukuaji wa mji wa Dodoma ni kubwa hivyo kuna haja ya kutafuta namna ya kuchangamanisha ukuaji wa mji na maendeleo ya sekta ya mifugo.
Mmoja wa wadau wa Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) akipokelewa na kusajiliwa kwa ajili ya kushiriki Kongamano hilo linalofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba 2- 4, 2020.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amos Zephania akiongea na washiriki (hawapo pichani)
wakati akifungua Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa
Mifugo na Uvuvi na Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji
na Uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) unaofanyika jijini Dodoma kuanzia
Desemba 2- 4, 2020.
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Amos Zephania (katikati waliokaa) akiwa katika picha
ya pamoja na sehemu ya Washiriki wa Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji
na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha
Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) unaofanyika
jijini Dodoma kuanzia Desemba 2 - 4, 2020. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
TSAP, Dkt. Imna Malele, wapili kutoka kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy na watatu ni Mwenyekiti wa
TSAP, Dkt. Daniel Komwihangilo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dkt. Jonas Kizima, wapili ni
Kaimu Mkurugenzi, Uzalishaji na Masoko, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen
Michael na watatu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Uwekezaji (TIB), Dkt. Maria
Mashingo.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wataalamu wa Mifugo Tanzania (TSAP), Dkt. Daniel Komwihangilo akieleza jambo
katika Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na
Uvuvi na Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na
Uendelezaji wa MifugoTanzania (TSAP) unaofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba
2 - 4, 2020.
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Dodoma, Maduka Kessy akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika Kongamano
la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na Mkutano
wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo
Tanzania (TSAP) unaofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba 2- 4, 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji
na Masoko, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael akitoa hoja katika
Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na
Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa
Mifugo Tanzania (TSAP) unaofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba 2- 4, 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wataalamu wa Mifugo Tanzania (TSAP), Dkt. Daniel Komwihangilo (kushoto)
akimkaribisha mmoja wa washiriki wa Kongamano la 43 la Kisayansi la Uzalishaji
na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi na Mkutano wa 44 wa mwaka wa Chama cha
Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) unaofanyika
jijini Dodoma kuanzia Desemba 2- 4, 2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni