Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2020

DKT. TAMATAMAH AKABIDHI INJINI ZA BOTI KWA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAVUVI KANDA YA ZIWA VICTORIA.

Picha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akikabidhi Injini ya Boti kwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Zilagula, Bi. Agness Mbasha katika hafla fupi ya kugawa Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa Victoria iliyofanyika katika Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020) Pichani ni Injini za Boti (4) aina ya Yamaha ambazo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezikabidhi kwa Vyama vinne (4) vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa Victoria katika hafla fupi iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020) Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, Dkt. Erastus Mosha (kushoto) muda mfupi kabla ya kukabidhi Injini za Boti kwa Vyama vya Ushirika vya Wavuvi Kanda ya Ziwa Victoria katika hafla fupi iliyofanyika Wilayani Muleba, Mkoani Kagera. (23.10.2020) Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Huduma za U...

PROF. GABRIEL AFUNGA MAFUNZO YA SIKU MBILI YA WAKAGUZI WA VYAKULA VYA MIFUGO

Picha
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendelezaji Maeneo ya Malisho na Rasilimali za vyakula vya Mifugo (WMUV), Bw. Rodgers Shengoto akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi kuhusu mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ya siku mbili ya wakaguzi wa vyakula vya Mifugo kwa Kanda ya Mashariki na Kati, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (23.10.2020) Washiriki wa mafunzo ya ukaguzi wa vyakula vya Mifugo wakisikiliza kwa makini mgeni rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), mkoani Morogoro. (23.10.2020) Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo (WMUV), Dkt. Asimwe Rwiguza akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi kuhusu mafunzo ya siku mbili ya wakaguzi wa Vyakula vya Mifugo wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo ...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

WATUMISHI WATAKIWA KUZIFAHAMU SHERIA NA TARATIBU ZA UTUMISHI WA UMMA.

Picha
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Zachariyya Kera amewataka watumishi wa umma kujijengea tabia ya kusoma katiba na sheria za kiutumishi ili kuzifahamu sheria na haki zao za msingi.   Akiongea wakati alipotembelea ofisi za Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) (20.10.2020) zilizopo Mkoani Pwani, akiambatana na baadhi ya viongozi waandamizi wa wizara hiyo sekta ya mifugo, Bw. Kera ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka   wafanyakazi kujua haki zao za msingi na kufuatilia kwa wakati.   "Watumishi waelimishwe kuhusu haki zao na wapate stahiki zao kwa wakati na kujijengea tabia ya kusoma sheria na taratibu za kiutumishi ili wasipitwe na mambo mengi." alisema Bw. Kera.   Katika ziara hiyo ya baadhi ya viongozi waandamizi wa Wizara ya Mifugo na uvuvi sekta ya mifugo, walipata pia fursa ya kutembelea kituo cha uhimilishaji kanda ya mashariki (kibaha) kilichopo Mkoani humo na Shamba ...

DKT. TAMATAMAH AKABIDHI VIPANDE VYA KAMBA 700,000 KWA WAKULIMA WA MWANI

Picha
  Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah amekabidhi vipande vya kamba za manila 700,000 kwa wakulima wa mwani katika Kijiji cha Songosongo, wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi.   Akizungumza na wananchi wa Songosongo jana (19/10/2020) Dkt. Tamatamah amesema serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) imetoa kamba hizo ili kuwawezesha wakulima wa mwani kwani kamba ilikuwa ni moja ya changamoto waliyokuwa wakikabiliana nayo.   Kamba hizi za manila (ambazo kila moja ina urefu wa mita 10) katika kilimo cha mwani, hufungwa katika vigingi na hutumika kwa ajili ya kuoteshea mwani ambapo mwani hufungwa katika kamba hizo zinazosaidia pia mwani kutochukuliwa na maji ya bahari pale panapokuwepo na wimbi.   Dkt. Tamatamah amesema duniani kote kwa sasa mwani unalimwa kibiashara, hivyo mwani ni moja ya zao linalopewa kipaumbele katika wizara. Katika kilimo cha mwani wakulima wanakutana na changamoto mbalimbali zikiwemo za ukosefu...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

SEKTA YA UVUVI INATOA ASILIMIA 30 YA PROTINI KWENYE LISHE - DKT. TAMATAMAH

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amewataka wafugaji na wavuvi nchini kuacha kufanya kazi zao kwa mazoea na badala yake watumie njia za kisasa na kitaalam katika utekelezaji wa shughuli hizo.   Dkt. Tamatamah aliyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa za Sekta za Mifugo na Uvuvi wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula duniani uliofanyika leo (10.10.2020) mkoani Njombe.   Katika taarifa yake Dkt. Tamatamah alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatambua umuhimu wa lishe bora kwa wananchi hususan wazee na watoto hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa nyama na samaki ni vyakula vinavyotoa protini kwa wingi zaidi ukilinganisha na vyakula vingine.   "Mhe. Mgeni rasmi sekta ya uvuvi inachangia asilimia 30 ya protini inayotokana na wanyama huku ikichangia ajira kwa Watanzania takribani Milioni 4.5 katika shughuli mbalimbali za sekta hiyo" Alisema Dkt.Tamatamah.   Aidha aliongeza kuwa uzalishaji wa samaki kwa ...

PROF. GABRIEL: OGESHENI MIFUGO YENU ILI KUIKINGA NA MAGONJWA

Picha
Wafugaji hapa nchini wametakiwa kuogesha mifugo yao ili kuikinga na magonjwa yaenezwayo na kupe.   Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel jana tarehe 10.10.2020 wakati akizindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo iliyofanyika katika Kijiji cha Bahi Sokoni, wilayani Bahi, mkoani Dodoma.   Prof. Gabriel amesema lengo kuu la kampeni hizi ni kuhamasisha wafugaji wote nchini kuunga mkono juhudi za serikali katika kuongeza tija ya ufugaji kwa kuwa na mifugo yenye afya njema, mifugo isiyo na magonjwa ambayo itazalisha mazao zaidi na yenye ubora wa kiwango cha kitaifa na kimatifa.   “Lengo la uogeshaji ni kudhibiti magonjwa yaenezwayo na kupe hususani Ndigana kali (East Coast Fever – ECF), Ndigana Baridi (Anaplasmosis), Mkojo Mwekundu (Babesiosis) na Maji Moyo (Heart Water) ambayo yamekuwa yakiathiri mifugo na kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji,” alisema Peof. Gabriel.   Magonjwa yaenezwayo na ...

IDARA YA UVUVI YAHAKIKISHA RASILIMALI ZA BAHARI ZINALINUFAISHA TAIFA KIUCHUMI

Picha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema ukusanyaji wa takwimu za sekta ya uvuvi katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi unalenga kutoa tathmini ya hali ya uvuvi katika ukanda huo na kuhakikisha rasilimali za bahari zinaendelea kuleta manufaa na kuchangia katika uchumi wa nchi. Akizungumza jijini Dar es Salaam (09.10.2020) wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya ukusanyaji wa takwimu za uzalishaji wa mazao ya uvuvi katika Ukanda wa Pwani yanayohusisha maafisa uvuvi na viongozi kutoka Vikundi vya Kusimamia Rasilimali ya Uvuvi Mwaloni (BMU), kutoka Mikoa ya Dar es Salaam katika Wilaya za Kinondoni, Kigamboni na Ilala pamoja na Mkoa wa Pwani ukihusisha Wilaya za Bagamoyo na Chalinze, Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi Bw. Emmanuel Bulayi amesema maendeleo ya wananchi katika eneo hilo yanategemea sana shughuli za uvuvi. “Kwa hiyo suala la kuchukua takwimu na kujua rasilimali ikoje kila wakati na kila muda ni suala la msingi sana ni ukweli uliowazi maendeleo ya wananchi katika hili eneo yanategemea...

SAUTI YETU WIKI HII

Picha
 

TAKWIMU SAHIHI ZA UVUVI, CHANZO KIKUU CHA KUTUNGA SERA NA MIPANGO YA MAENDELEO NCHINI

Picha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Idara ya Maendeleo ya Uvuvi imesema ni muhimu kuwa na watu wenye uelewa wa kukusanya takwimu za uvuvi ili kuhakikisha watunga sera wanakuwa na vigezo mbalimbali vya kutunga sera na mipango ya maendeleo nchini.   Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (08.10.2020) katika mafunzo ya siku mbili ya ukusanyaji wa takwimu za uzalishaji wa mazao ya uvuvi katika Ukanda wa Pwani yanayohusisha maafisa uvuvi na viongozi kutoka Vikundi vya Kusimamia Rasilimali ya Uvuvi Mwaloni (BMU), kutoka Mikoa ya Dar es Salaam katika Wilaya za Kinondoni, Kigamboni na Ilala pamoja na Mkoa wa Pwani ukihusisha Wilaya za Bagamoyo na Chalinze, Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Upendo Hamidu amesema kusipokuwa na takwimu sahihi za uvuvi ni vigumu kutunga sera pamoja na kuweka mipango ya maendeleo.   “Ili kuhakikisha kwamba takwimu za uvuvi zinakusanywa na zinatoa yale matunda ambayo yanategemewa na wizara inayatimiza, katika suala la takwimu k...